Na Karoli Vinsent
KAMPUNI ya Simu za Mkononi nchini ya Tigo kwa
kushirikiana Benki ya NMB leo wamezindua huduma mpya ya kifedha
ambayo itawalahisishia wateja wa Benki ya NMB pamoja na watumiaji wa mtandao wa
Tigo katika kutoa na kuweka Fedha kutumia simu ya mkononi.
Uzinduzi huo ulifanyika leo Jijini
Dar es Salaam na kushudiwa na Waandishi wa Habari Pamoja viongozi wa juu Benki
ya NMB na kampuni ya simu ya Tigo ,Akizungumzia Faida za huduma hiyo Meneja wa
Banki ya NMB ,Tom Borghol alisema huduma hii italeta mapinduzi ya Banki Nchini
na kukuza hali za maisha kwa wateja wa Banki hiyo pamoja na wateja wa Tigo.
ENDELEA HAPA---------
“kupanuliwa kwa huduma hii ya kuweka
fedha na kutoa fedha kwa njia ya Simu itawasaidia wateja zaidi ya milioni moja
waliojiunganisha na NMB mobile kwa sasa, mteja wa Nmb anaweza kutoa na kuweka pesa
kwa Wakala wa tigo pesa”alisema Borghol
Ikumbukwe kwa sasa
kuna Mawakala wa Tigopesa zaidi ya 20000,waliotapakaa Tanzania nzima pamoja na
pemba na Zanzibar
Mr Borghol alisema kwa huduma hii mpya
ya kutoa na kuweka Fedha kwenye Banki ya Nmb imetokana uhusiano mzuli uliopo
kati ya Banki ya Nmb pamoja Mtandao wa Simu za Mkononi Nchini wa Tigo na kuwepo
kwa huduma hii itasaidia kukuza uchumi wa nchi ya Tanzania na pia itarahisisha
kwa wateja kutuma pesa kwenda vijijini.
Kwa upande wake Meneja Biashara wa Tigo
Pesa, Ruan Swanepoel alisema huduma hii iliyozinduliwa ni miongoni mwa mikakati
inayofanywa na kampuni hiyo ya simu hapa nchini katika kuwajali wateja wake.
“Huduma hii tulioizindua leo ni huduma bora
sana na itawaondorea adha waliokuwa wanaipata wakati wa kutoa fedha kwenye
Banki, lakini kuwepo kwa huduma hii sasa Mteja wa Banki ya Nmb atatumia simu
yake ya mkononi kutoa fedha na kuweka fedha”
“Uzinduzi wa leo ni mwenderezo wa kampuni
hii simu katika kuwajali wateja wake na sasa tumeamua kuwasogezea huduma ya
kibenki kwenye simu zao za mkononi”alisema Swanepoel.
No comments:
Post a Comment