TAARIFA
YA MHE. BERNARD K. MEMBE (MB.), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA
KIMATAIFA ALIYOITOAKWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI ULIOFANYIKA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
TAREHE 20 FEBRUARI, 2014.
ENDELEA HAPA------------
1.
KUCHAGULIWA
TENA KWA TANZANIA KWENYE BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA (AU)
Tanzania
imechaguliwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa Mjumbe wa Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika (PSC) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia
mwaka huu. Tanzania ilichaguliwa kwa mara ya kwanza katika Baraza hilo mwaka
2012.
Miongoni mwa sababu muhimu
zilizopelekea Tanzania kuchaguliwa kwa mara nyingine kwenye Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika ni pamoja na:-
a.
Heshima
iliyojijengea kimataifa, hususan katika utatuzi wa migogoro ya kikanda kama ile
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Madagascar;
b.
Tanzania
imekuwa mstari wa mbele kuchangia vikosi vya kulinda amani kwenye maeneo mbalimbali yenye migogoro kama
vile Darfur, DRC, Lebanon n.k;
c.
Kuaminika kwa
vikosi vya Tanzania vinapopelekwa kulinda amani kwa sababu ya ujuzi, nidhamu na
kujituma.
TANZANIA
YAJIJENGEA HESHIMA
Mbali na kupata fursa adimu
ya kushughulikia moja kwa moja masuala nyeti ya amani na usalama Barani Afrika,
uanachama wa Baraza la Amani utaijengea Tanzania heshima kubwa hapa Barani na
Kimataifa.
2.
VIKOSI
VYA KULINDA AMANI KUTOKA TANZANIA
Tanzania
imekuwa mstrari wa mbele katika masuala mbalimbali yanayohusu harakati za
ukombozi duniani. Tanzania imekuwa pia mstari wa mbele kuchangia vikosi vya
kulinda amani kwenye maeneo mbalimbali yenye migogoro Barani Afrika na
kwingineko. Hadi sasa Tanzania ina vikosi vya askari huko Lebanon na askari
huko Darfur, Sudan. Aidha, Tanzania ilishiriki kikamilifu katika kufikia uamuzi
wa kutuma Kikosi cha Kulinda Amani cha SADC nchini DRC.
Tanzania
ilikuwa ni nchi ya kwanza kujitolea kutoa Kikosi Kimoja cha Wanajeshi (Force
Intervention Brigade-FIB) huko Mashariki mwa DRC. Wanajeshi kutoka Tanzania ni
takriban 1,283 kati ya Wanajeshi 3,069 kutoka Afrika Kusini na Malawi. FIB kwa
kushirikiana na vikosi kutoka Afrika Kusini, Majeshi ya Serikali ya DRC na Vikosi
vya MONUSCO mwezi Desemba 2014 walifanikiwa kukisambaratisha Kikosi cha Waasi
cha M23 na kuwezesha amani Mashariki mwa Kongo kurejea tena.
3.
MGOGORO
WA TANZANIA NA MALAWI KUHUSU MPAKA KWENYE ZIWA NYASA
Mgororo
huu kwa sasa uko chini ya usuluhishi wa Mhe. Joachim Chissano, Mwenyekiti wa
Jopo la Usuluhishi wa Jukwaa la Viongozi Wastaafu wa Afrika Ukanda wa SADC.
Mnamo
tarehe 27 Novemba, 2013 Tanzania na Malawi ziliwasilisha utetezi wa hoja zao
kwa Mwenyekiti wa Jopo la Usuluhishi ilikuliwezesha Jopo hilo kutafakari hoja
za pande zote mbili na kutoa uamuzi/ushauri wake kuhusu mgogoro huo.
Kwasasa
Tanzania na Malawi zinasubiri kuitwa na Jopo hilo ili kwenda kupokea
ushauri/uamuzi wa jopo hilo kuhusu mgogoro huo.
Tanzania
inapenda kuiomba Malawi kuendelea kutoa ushirikiano hadi hapo suala hili
litakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu.
4.
MGOGORO
WA SUDAN KUSINI
Sudani Kusini ilikumbwa na mapigano mkubwa katikati
ya Mwezi Desemba 2013 kati ya vikosi vya serikali na waasi, ambao wanamuunga
Makamu wa Rais wa zamani Bw. Riek Machar. Mapigano hayo yalizuka baada ya Rais
Kiir kumtuhumu Bw. Machar kufanya Jaribio la kupindua Serikali.
Mapigano
hayo yalichukua sura ya ukabila kati ya kabila la Dinka analotoka Rais Kiir na
kabila la Nuer ambalo Bw. Machar anatoka. Hadi sasa zaidi ya watu 1000 wameuawa
na 700,000 kulazimika kukimbia makazi yao. Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na
IGAD iliingilia kati na kuanzisha mazungumzo baina ya pande hizo mbilli.
Kufuatia
mazungumzo hayo, tarehe 2013 Januari 2014 pande hizo mbili zilisaini Mkataba wa
Kusitisha Mapigano mjini Addis Ababa, baada ya Serikali kukubali kuachia
wafuasi 7 kati ya 11 wa Bw. Machar, ambao Serikali ilikuwa ikiwashikilia kwa
tuhuma za kupanga Mapinduzi.
Duru
ya Pili ya mazungumzo kati ya pande hizo ilianza tarehe 10 Februari, 2014 kwa
lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo. Upande wa waasi bado
unasisitiza kuachiliwa kwa wafuasi 4 waliobaki. Aidha, Waasi wanataka majeshi
yote ya nje yaliomo nchini humo kuondoka mara moja.
Wakati
mazungumzo hayo yakiendelea, kulikuwepo na taarifa za mapigano ya kushitukiza
baina ya Vikosi vya Serikali na Vikundi vya waasi kwenye baadhi ya maeneo ya
nchi hiyo. Tarehe 18 Mwezi huu, mapigano mapya yameibuka katika jimbo la Upper
Nile ambapo pande zote zinashutumiana kuvunja makubaliano ya kisitisha
mapigano.
Kwa
upande wake Vikosi vya Umoja wa Mataiifa (UNMISS), ambavyo mwezi Desemba 2013
idadi yake iliongeka kutoka 7000 hadi 12,500 vimeendelea na jitihada za
kuimarisha amani. Tunaomba kuchukua fursa hii, kutaarifu kuwa Tanzania imeahidi
kuchangia vikosi vyake kujiunga na jeshi hili la Umoja wa Mataifa lililoko
Sudani Kusini. Pamoja na kuchangia vikosi hivyo Tanzania inaomba pande
zinazopigana kusitisha mapigano na kuendelea na mazungumzo ili kupata suluhu ya
kudumu ya Mgogoro huo.
5.
UHUSIANO
WA TANZANIA NA RWANDA
Kama itakavyokumbukwa vyombo vingi vya habari
viliripoti kudorora kwa uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda. Baada ya
mazingumzo kati ya Rais Kikwete na Rais
Kagame yaliofanyika Mjini Kampala mwezi Septemba, 2013 hali ya uhusiano wetu
iliboreka.
Hata
hivyo hivi karibuni vyombo ya habari vya Rwanda lilikiwemo Gazeti la Serikali
la “News of Rwanda” Vimetoa taarifa
za kuishutumu Tanzania na viongozi wake. Aidha kumekuwepo na taarifa za
kuishutumu Tanzania kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani nchini Rwanda
akiwemo ambapo Waziri Mkuu wa zamani wa Rwanda, Bw Faustine Twagiramungu.
Serikali
ilijibu shutuma hizo kwa kueleza kuwa Tanzania haisaidii vikundi vyovyote vya
waasi na pia haijawahi kufanya mazungumzo wala kuwakaribisha viongozi wa
Upinzani wa Rwanda.
Historia
ya Nchi yetu tangu uhuru inajulikana kuwa tumekuwa tukisisitiza Amani Barani
Afrika na hivyo hatuna sababu yoyote wa kusaidia waasi ili kuchochea migogoni.
Hivyo, tunaomba kuchukua nafasi hii kuwaonya wale wote wanaotaka kuchafua sifa
nzuri ya Tanzania kuacha mara moja. Aidha tunawaomba wanahabari kutoshabikia taarifa
hizi za uzushi.
Tanzania
siku zote inataka uhusiano mzuri na jirani zake lakini tusingependa kupenda
Amani kwetu kuwe ndiyo sababu ya watu kutaka kutuchafua.
6.
URAIA
WA NCHI MBILI (DUAL CITIZENSHIP) UTAMBULIWE NA KATIBA MPYA
Kama
mnavyofahamu, Bunge Maalum la Katiba limeanza vikao vyake Mjini Dodoma tarehe
18 Februari 2014. Wizara iliratibu ushiriki wa Wanadiaspora katika Bunge hilo ili
sauti na maoni yao yaweze kujumuishwa katika Katiba Mpya.
Jitihada
hizo zimemwezesha mmoja wa Wanadiaspora, Bw.
Kadiri Singo kuteuliwan na Mhe. Rais Kikwete, ili kuweza kushiriki kikamilifu. Bw. Singo ameshawasili nchini na kusajiliwa, tayari kushiriki katika Bunge hilo la Katiba Mpya.
Tunataka
Katiba ielekeze kutungwa kwa sheria ya uraia itakayofafanua vigezo na masharti
kuhusu haki na wajibu wa Raia wa Tanzania mwenye uraia wa pili; Katiba itamke
kuwa raia wa kuzaliwa wa Tanzania hatapoteza uraia wake kwa sababu tu amepata
uraia wa nchi nyingine na Katiba ilinde haki ya uraia wa kuzaliwa kwani ni haki
ya msingi ambayo haitakiwi kuvuliwa na mamlaka yoyote ile.
FAIDA ZA URAIA WA NCHI MBILI
Tafiti
zinaonesha kuwa, Uraia wa Nchi Mbili ni nguzo kuu ya kuandaa mazingira nje ya
nchi kuwawezesha raia hao kustawi kielimu, kiafya, kiuchumi, kijamii na kisiasa
kama ifuatavyo:
i.
Elimu:
Elimu ni chimbuko la mafanikio. Uraia wa Nchi mbili utawawezesha kusoma katika
shule za Serikali, kulipa ada za chini za raia na kupata ufadhili wa masomo
(scholarships).
ii.
Ajira:
Kupata ajira zenye staha (decent employment). Nchi nyingi hutoa ajira nzuri (au
katika sekta rasmi) kwa raia pekee hata kama mgeni amesoma na kuwa na sifa sawa
au za juu zaidi. Vile vile watanufaika na malipo na huduma zingine uzeeni
wakiwa kama raia.
iii.
Afya:
Afya katika nchi nyingi ni gharama kubwa
sana hasa kwa wageni. Kama raia, Watanzania nje ya nchi watanufaika na huduma
za afya.
iv.
Uchumi:
Kama raia, atakuwa na uwezo wa kujishughulisha na masuala ya
kiuchumi kwa upana zaidi, kama kupata mitaji mikubwa, kupata mikopo katika
taasisi za fedha, kupata zabuni za kibiashara, kumiliki ardhi na mali nyingine
ambazo ni kwa raia pakee.
Ushawishi na kuitangaza nchi: Kama
raia, Watanzania ughaibuni watakuwa na fursa nzuri na uwezo wa kuisemea
Tanzania na kuvutia wawekezaji.
UHAMASISHAJI WA JAMII
KUHUSU DIASPORA
Wizaraya
Mambo yaNje, kupitia Idara yake ya Diaspora imeanza mchakato wa kuhamasishawa na
nchi na kutoa elimu kuhusu masuala ya Diaspora.
Hivi sasa, Wizara itaanza kushirikiana na Vyombo vya Habari (radio,
televisheni na mitandao ya kijamii) kuongelea umuhimu wa Diaspora katika kukuza
uchumi wa Tanzania.
Wizara
inasisitiza kuwa taifa lina jukumu la kulinda haki za Watanzania waishio nje kama
linavyowajibika kwa raia wanaoishi nchini.
7.
MKUTANO
KUHUSU KUPINGA BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI ULIOFANYIKA LONDON, UINGEREZA
Mhe. Rais Jakaya
Mrisho Kikwete alihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa kuhusu biashara haramu ya
wanyamapori. Mkutano huu ulifanyika jijini London, Uingereza kuanzia tarehe
12-13 Februari 2014. Mkutano huu uliandaliwa na serikali ya Uingereza na
ulichagizwa na juhudi za Mwanamfalme Charles pamoja na wanae William na Harry
katika kushughulikia tatizo hili.
Mkutano
uliikutanisha jumuiya ya kimataifa kwa lengo la kujadili na kutafuta mbinu za
kumaliza kabisa biashara hii haramu hasa ya pembe za ndovu na faru. Biashara
hii imekua sana siku za karibuni hasa kutokana na kuongezeka kwa soko la pembe
za ndovu na faru katika nchi za Asia. Uchunguzi wa kimataifa umeonyesha kuwa
biashara hii imechukua sura ya kimataifa na kushirikisha magenge ya Kimataifa
ya kihalifu kutokana na kuwa na faida kubwa sana.
Kutokana na
kushiriki kwa magenge ya kihalifu ya Kimataifa, biashara hii imehusishwa na
kufadhili shughuli za kigaidi, migogoro ya kisiasa na kijamii kwenye baadhi ya
maeneo hasa barani Afrika. Mwelekeo huu umeifanya jumuiya ya kimataifa kuanza
kuliangalia tatizo la ujangili sio tu kama tatizo la kiuhifadhi (conservation problem)
bali pia kama tatizo linalogusa usalama wa Kimataifa (international security).
Tanzania ni
miongoni mwa nchi ambazo zimeathirika sana na biashara hii kutokana na kuwa
tembo na faru wengi sana. Ujangili umekuwa ni tatizo sugu kwa nchi yetu tangu
enzi za Uhuru mpaka leo. Katika kipindi chote hiki, serikali imeendelea
kupambana vikali na majangili kuhakikisha wanyama hawa adhimu wanalindwa na
hawapotei katika ardhi yetu. Kwa mfano, baada ya Uhuru Tanzania inakadiriwa
ilikuwa na tembo 350,000, kutoka na ujangili uliokithiri katika miaka ya 1980
idadi yao ilishuka na kufikia tembo 55,000 tu mwaka 1987.
Serikali ya
wakati huo ikaanzisha operesheni iliyojulikana kama “Operesheni Uhai” ili
kupambana na ujangili. Oparesheni hii ilikuwa na mafanikio makubwa na mafanikio
haya yalichagizwa pia na marufuku ya biashara ya pembe za ndovu na faru
iliyoweka mwaka 1989 na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Biashara ya Wanyama
walio katika tishio la kupotea(CITES). Kutokana na haya, idadi ya tembo
iliongezeka maradufu na kufikia 110,000 mwaka 2009 na ujangili ukawa
umedhibitiwa kwa kiwango kikubwa.
Kutokana
na kupanuka sana kwa soko la bidhaa hizi hasa kwenye nchi za Asia miaka ya
karibuni, wimbi la biashara hii limerudi kwa kasi kubwa sana. Biashara hii
imerejea ikiwa na changamoto nyingi sana ikiwemo utumiaji wa mbinu za kisasa
kabisa za ujangili. Kama ilivyokuwa huko nyuma kumekuwa na juhudi kubwa sana
kwa upande wa serikali kuhakikisha kuwa hali hii, kama ilivyokuwa huko nyuma,
inadhibitiwa. Katika juhudi hizo, hivi karibuni Mhe. Rais aliridhia utumiaji wa
jeshi letu katika kupambana na kudhibiti biashara hii na hivyo “Oparesheni
Tokomeza” ikaanzishwa.
Kwa bahati mbaya
sana kumekuwa na upotoshwaji mkubwa wa juhudi za serikali za kupambana na
bishara hii haramu. Baadhi ya magazeti ya Kimataifa yamediriki kuihususha
serikali yetu na bishara hii eti kutokana na wao kutokuona uthabiti wa juhudi
za serikali kupambana na bishara hii. Tumeenda London kushiriki mkutano huu
tukiwa na mambo matatu ya msingi:-
i.
Tukiwa
miongoni mwa wahifadhi (custodians) wa tunu hii ya wanyama, tumeenda kuungana
na jumuiya ya Kimataifa kusaidia kutafuta mbinu za kudhibiti na kumaliza kabisa
bishara hii haramu na ambayo inatuathiri sana ukizingatia wanyama hawa nbi
kivutio kikubwa cha utalii ambao kwetu moja ya sekta zinazotuingizia fedha
nyingi za kigeni.
ii.
Kubadilishana
mbinu na kuweka kumbukumbu sawa kwa kuelezea juhudi ambazo serikali yetu
inazifanya katika kudhibiti biashara hii.
iii.
Kuomba
usaidizi wa kimataifa pale ambapo juhudi zetu binafsi zinakinzwa na uhaba wa
rasilimali, ukosefu wa mbinu za kisasa, ujuzi na uzoefu.
Mkutano ulikuwa
na mafanikio sana ambapo Mhe Rais alopata fursa ya kuhutubia. Katika hotuba
yake aliungana na viongozi wa kimataifa kupongeza juhudi za serikali ya
Uingereza kuitisha mkutano huu muhimu kwenye muda mnuafaka. Katika hotuba yake,
pamoja na kuelezea juhudi ambazo serikali yake inazifanya, alisisitiza umuhimu
wa kuhakikisha kuwa soko la bidhaa hizi huko katika nchi za Asia linatokomezwa
kabisa kama moja ya njia za kuimaliza biashara hii. Pia aliezea juhudi ambazo
serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya kuhakikisha kuwa tembo na faru waliopo
wanalindwa na wanapewa mazingira ya kuzaliana.
Mkutano
ulikubaliana pamoja na mambo mengine, kuongeza ushirikiano wa Kimataifa katika
kudhibiti bishara hii; kupiga marufuku ya jumla ya bishara hii kimataifa bila
kutoa ahueni (moratorium) kama ilivyokuwa inafanyika awali; kuhakikisha kuwa
nchi zinapitisha sheria kali dhidi ya ujangili na kuhakikisha kuwa hazina ya
meno yaliyohifadhiwa sasa hivi yanakosa thamani (putting stock pile beyond
economic use).
8.
MAANDALIZI
YA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA
Michezo ya
Jumuiya ya Madola (Commonwealth Games)
itafanyika Glasgow, Scotland kuanzia tarehe 23 Julai hadi 3 Agosti 2014.
Miongoni mwa
alama kuu za michezo hiyo ni Kifimbo cha Malkia (Commonwealth Queen’s Baton) ambacho hukimbizwa kwa nchi wanachama
wa Jumuiya ya Madola kuashiria kuanza kwa michezo hiyo. Kifimbo kicho kilikuja
hapa nchini kuaniza tarehe 18 hadi 20 Januari 2014 na kupokelewa na Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tukiwa na lengo
la kuitoa nchi yetu kimasomaso na kufanya vizuri kwenye michezo hiyo, Tuliiomba
Serikali ya Uturuki wanamichezo wetu waweke kambi nchini humo kwa ajili ya
kufanya maandalizi ya michezo hiyo. Uturuki imekubali ombi hilo. Kwa jitihada
hizi za serikali na jitihada za Tanzania Olympic Committee (TOC), pamoja na
zile za wanamichezo wenyewe tunategemea wanamichezo wetu watafanya vizuri
kwenye mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment