Tuesday, March 25, 2014

BAADA YA KULISAFISHA JIJI WIKI ILIYOPITA,MSANII ROSE NDAUKA AJA NA TAMASHA BAB KUBWA TANZANIA,SOMA HAPA

Msanii maarufu wa filamu tanzania ROSE NDAUKA katikati akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam


Na Karoli Vinsent

        BAADA ya kuwaacha Midomo wazi wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika kujitolea kufanya usafi wa kufagia Barabara za jiji hilo,Staa filamu Nchini Rose Ndauka ameandaa Tamasha kubwa litakalowafanya wapenzi wa burudani nchi kufurahia.

       Hayo,yametangazwa leo Jijini Dar es Salaam na Rose Ndauka wakati wa mkutano na waandishi Habari ambapo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye Tamasha hilo.

       “Nawasihi wananchi hususani wa Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi kwenye Tamasha hili la Burudani ambalo litafanyika ijumaa ya Tarehe 28 mwezi huu saa kumi nambili jioni katika viwanja vya chuo cha utalii kilichopo Posta karibu na wizara ya afya na kukaribiana na chuo cha usimamizi wa Fedha IFM”

       “Tamasha hili litakuwa na Burudani nyingi zitakazokufanya ufurahi ikiwemo kutoka kwa msaniii Leah Muddy ambae ni mshindi wa shindano la bongo star search pamoja na vikundi vya ngoma za asiri “alisema Ndauka


Rose Ndauka ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wasanii bora wa kike kwa upande wa Filamu hapa nchini na Afrika mashariki na Kati alisema kiingilio katika tamasha hilo ni  cha chini kitakachomfanya kila mtanzania kushiriki.
“Tumeamua kuweka kiingilia cha sh 35000 za kitanzania ili kumfanya kila mtanzania kushiriki katika tamasha hili na vilevile katika Tamasha hili kutakuwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Balozi wa Kenya hapa nchini pamoja viongozi wengine wa Nchi”alizidi kusema Ndauka

          Katika Tamasha hilo atakuwepo Poul masati ambaye atakuwa Mshereheshaji katika tamasha hilo pamoja na Felix mganjira nae atatoa mada mbalimbali katika tamasha hilo.

Huu ni mwenderezo wa Star huyo wa Firamu kwa upande wa Kinadada kufanya kitu cha pekee hapa nchini.


No comments: