Afisa mahusiano wa kampuni ya tigo tanzania JOHN WANYANCHA akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam
Tigo Tanzania leo imetangaza
udhamini wake kwa maonyesho ya biashara yajulikanayo kama ‘Kariakoo @ Coco
Beach Shopping Festival’ yenye malengo ya kuinua biashara za wafanyabiashara kutoka
Kariakoo.
Akitangaza udhamini huo
kwa waandishi wa habari kutoka ukumbi wa Coco Beach jijini Dar es Salaam,
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha, alisema maonyesho hayo ambayo yatafanyika
kila mwisho wa mwezi yana malengo ya kuleta bidhaa zenye gharama nafuu kutoka
Kariakoo mpaka ufukwe wa bahari wa Coco kwa ajili ya kuwaondolea wateja usumbufu
wa kwenda mpaka mjini na kero ya msongamano wanayoipata wakiwa huko.
“Ukiondoa mazingira mazuri
ambayo maonyesho haya yatawapatia wateja, pia tunaamini ya kwamba kupitia maonyesho
haya wafanyabiashara wakati na wadogo wote watafaidika na kutokana na wateja watakaokuja
kununua bidhaa zao, hivyo kuwasaidia kuongeza mauzo yao na hatimaye kukuza biashara
zao,”alisemaWanyancha.
Wanyancha aliendelea kusema
kwamba wauzaji na wanunuzi watapata urahisi wa kuuza au kulipia bidhaaa huduma mbalimbali
kupitia Tigo Pesa na kwa gharama ileile ya bila makato yoyote.
Kutoka na na maelezo ya
waandaji wa maonyesho hayo, Hazina Capital, uzinduzi utafanyika Jumamosi na Jumapili
wikendi ijayo ya tarehe 29 na 30 Machi
2014, na kufuatiwa na maonyesho kama hayo yatakayofanyika kila wikiendi ya mwisho
wa mwezi.
|
No comments:
Post a Comment