Mwandishi huyo akitembelea hifadhi ya meno ya tembo |
NA KAROL VICENT
KILE kinachotafsriwa ni kugeukwa kwa
serikali ya Tanzania na Mwandishi wa Gazeti la Sunday Mail la Nchini uingereza
Martini Fletcher baada ya kuandika makala nyingine ikihishutumu tena
serikali ya Jakaya kikwete kwa kushindwa kuwachukilia hatua Majangili.
Kugeukwa kwa Serikali ya Tanzania
kumetokana na Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro
Nyalandu kutumia Garama kubwa ya kumuita Mwandishi huyo kile
kinachoonekana ni kujikosha kwa serikali baada ya mwandishi huyo kuandika
makala ikiituumu serikali ya Tanzania kushindwa kuwachukulia hatua Majangili.
Katika Makala yake hiyo ya
Jumapili ya Tarehe 23 mwezi huu alimshutumu Rais Kikwete kwa kushindwa
kuwachukulia Hatua Majangili huku akiwajua kabisa wanapokaa.
Makala hiyo ilizidi kusema Chama cha
Mapinduzi CCM ambacho ni Chama anachotoka Rais Kikwete ndio vinara wa Vitendo
vya ujangili, ,vilevile Ndio sababu Rais kikwete kushindwa kuwachukulia hatua
Majangili.
Ikumbukwe Mwandishi huyo aliwasili
nchini wiki mbili zilizopita na kufikia kwenye hoteli ya Kimataifa ya Serena na
Baadae kutembelea pori la akiba Selous na Hifadhi ya Serengeti.na vilevile
inasemekana alionana na Rais wa Jakaya kikwete ili Mwandishi huyo abadili kile alichokiandika
kwenye makala yake.
Makala ya Fltecher kwenye Gazeti hilo
la Uingereza,yaliwakasirisha viongozi wa Tanzania hususan Rais Kikwete hasa
kutokana na ujio wake ulilenga muda ambao viongozi wa mataifa zaidi ya 50
walikuwa wamealikwa kwenye mkutano maalum ulioitishwa na mwana wa Mfalme wa
Uingereza,Prince Charles,mjini London
Makala yake aliyoitoa Februali 8
mwaka huu na kuchapishwa kwenye Gazeti la Sunday Mail ambapo katika makala hiyo
ilimtuhumu Rais kikwete kwa kushindwa kuwachukulia hatua vinara wa vitendo vya
ujangili
Vilevile, Makala hiyo ikizidi
kumtuhumu Kikwete kwa kumdharau aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii Barozi
Khamisi Kagasheki alipokuwa anamletea Orodha ya vinara wa vitendo vya ujangili.
Baada ya kuandika Makala hiyo
Rais Kikwete wakati alipokuwa nchini uingereza anahojiwa kwenye kituo cha
televishieni cha CCN alikanusha taarifa hiyo na kusema serikali yake imefanya
kazi kubwa ya kukomesha vitendo vya ujangili hapa nchini.
Duru za mambo zinasema kugeukwa kwa
Serikali ya Tanzania na Mwandishi huyo,kunaonyesha udhaifu kwa serikali katika
kusimamia mambo huku wengine wakisema Kuna haja gani ya Serikali kutumia pesa
nyingi sana kumleta mwandishi huyo ili andike makala nyingine ya kuisafisha
Serikali ya Tanzania,Badala ya kuwachukulia hatua majangili,
Huu ni mwendelezo wa Serikali ya Jakaya
Kikwete kuwadaa watanzania ikumbukwe wakati anahutubia Bunge Rais Kikwete
aliwaikujinadi kuwa anaorodha ya Vinara ya wauza madawa ya Kulevya lakini
alishindwa kuwachukulia hatua
No comments:
Post a Comment