Makatibu wakuu wa vyama vya CHADEMA,CUF,NA NCCR MAGEUZI wakizungumza na wanahabari jijini dar es salaam baada ya kutangaza muungano wao wa kupinga mambo ambayo yanaendelea bunge maalum la katiba |
Mungano
wa vyama vitatu vya upinzani vyenye wabu nge bungen ambao kwa sasa unajiita
umoja wa katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza kufanya mikutano ya hadhara
kiwa mikoa yote Tanzania kupinga kile ambacho wanakiita kuhujumiwa kwa mchakato
wa kupata katiba mpya ambao wanaituhumu moja kwa moja ccm kuwa wanataka
kuhujumu mchakakato wa kupata katiba mpya.
Akitangaza maamuzi hayo ambayo ni ya makatibu wakuu
wa vyama vya CUF,NCCR MAGEUZI NA CHADEMA,katibu mkuu wa CHEDEMA dk WILBROD SLAA
wakati wa mkutano na wanahabari katika katika makao makuu ya CHADEMA amesema
kuwa ukawa imekuwa ikifanya kazi ndani ya bunge na sasa wameunda UKAWA nje ya
bunge ili kuwasaidia wale waliopo bungeni kuwaletea watanzania katiba ya
wananchi na siyo ya ccm.
Dk SLAA anasema kuwa UKAWA NJE wameamua kuwafuata wananchi wa Tanzania kuwaunganisha
nguvu zao na kuwaeleza ukweli juu ya mchakato wa katiba mpya unavyotekwa na ccm
na kufanya wabunge wa bunge maalum la katiba wanaotaka katiba ya wananchi kuonewa
ndani ya bunge na kutokutendewa haki katika bunge hilo.
Anasema kuwa UKAWA NJE watafanya mikutano ya hadhara nje na ndani
kwa nchi nzima ambapo kampeni hiyo wametangaza kuizindua kesho mkoani mwanza na
baadae kufanyika kila mkoa wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CHADEMA DK WILBROD SLAA akizungumza kwa niaba ya makatibu wakuu wenzake katika mkutano na wanahabari jijini dar es salaam muda mfupi uliopita |
No comments:
Post a Comment