KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA
MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HENRY JUMA MKAZI WA
MIGOMBANI ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KULAZWA KITANDANI
NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA VENANCE.
TUKIO HILO LA KUSIKITISHA
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA
KATA YA MIGOMBANI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA AMBAPO BAADA YA
UHALIFU HUO, MTUHUMIWA ALIFUNGA MLANGO KWA NJE NA KUFULI NA KUTOKOMEA
MAHALI KUSIKOJULIKANA. WAPELELEZI PAMOJA NA RAIA WALIPOVUNJA MLANGO NA
KUINGIA NDANI WALIKUTA MAITI YA MTOTO HUYO IKIWA KITANDANI. KATIKA
CHUMBA HICHO WALIKUTA UJUMBE WA MANENO MENGI YALIYOANDIKWA NA MTUHUMIWA,
BAADHI YA MANENO HAYO NI “UNYAMA UNYAMANI, TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI”. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
|
Monday, March 24, 2014
BABA AMNYONGA MWANAE MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA KISHA KUACHA UJUMBE TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment