Bunge maalum la katiba Limekutana Jioni Hii kuendelea na Shuguli
zake Lakini Mvutano Mkubwa Umejitokeza Hali iliyosababisha Vurugu
Iliyoambatana na Kuzomea Zomea,Mvutano Huo Uliibuka Pale Mjumbe Mh. Tundu Lissu Aliposimama kuomba Muongozo Kuhusu Marekebisho ya Kanuni Ambayo anamtuhumu Mwenyekiti wa Bunge Mh Samweli Sitta Kupitia Kamati ya Uongozi kuleta Marekebisho Ya Mabadiliko ya kanuni Kinyume cha Kanuni zilizopitishwa na Bunge Hilo la Katiba Wakati wakijadili na Kupitisha Kanuni za Bunge Hilo.
Mwenyekiti wa Bunge Hilo Mh Samweli Sitta Aliingilia Kati kujaribu Ufafanuzi Pamoja na Wajumbe Wengine Akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh Jaji Fredrick Werema
Lakini hali ya Kuzomea Iliendelea Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Hilo
Alipolazimika Kuliahirisha Bunge Hilo Mpaka Kesho na Kuamuru Mapendekezo
ya Mabadiliko HayoMabadiliko hayo Yapelekwe kwenye Kamati Ya Kanuni
Kajili ya Maamuzi ili Yaweze Kuwasilishwa Katika Bunge Hilo. |
No comments:
Post a Comment