Na Mwandishi Wetu.
BENKI
ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi zawadi ya gari jipya aina ya
Suzuki Swift kwa mshindi wa kampeni ya Weka Upewe iliyomalizika hivi
karibu kwa mkazi wa Kigoma B. Mary Malifedha Popote jijini Dar es Salaam
jana.
Akizungumza
wakati akikabidhi gari hilo lenye thamaninya dola za kimarekani 17,000,
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi. mizinga Melu alisema, kama benki
wamefurahi kuona kampeni hiyo ikimadiisha maisha ya wasindi 13
waliobahatika kujishindia zawadi mbalimbali.
"Tunaamini
zawadi hii gari itamsaidia huyu mteja wetu kubadilisha maisha yake
kwani itamsaidia kupunguza kero za usafiri au kulitumia kama njia ya ku
uongezea kipato", alisema.
Naye
Mkuu wa Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa wa NBC, Andrew Massawe
alisema kampeno hiyo iliyokuwa ikiwashiriksha wateja wao wenye akaunti
ya Malengo imepata mafanikio makubwa kutokana na muitikio kutoka kwa
wateja wao.
Alisema
kila mteja aliyekuwa na kiasi cha shs 50,000 au kuweka kiasi hicho cha
fedha katika akaunti yake ya Malengo aliweza kuingia katika kampeni
ambayo washindi walishinda zawadi mbalimbali kama pikipiki, jenereta za
umeme na zawadi hiyo kubwa ya gari.
"Kampeni
ya Weka Upewe imepata mafanikio makubwa kwani tumeshuhudia wateja wengi
wa akaunti ya malengo wakiongeza amana zao na wengine kujiunga, muda si
mrefu tutakuja na kampeni nyingine kabambe zaidi ili kuwafanya wateja
wetu wafurahi kuweka fedha zao katika benki yetu", alisema.
Naye
mshindi aliyejinyakulia gari hilo Mama Mary Malifedha Popote alisema
anaishukuru sana Ben ya NBC kwa zawadi hiyo kwani hakuweza kutegemea
yeye mkazi wa maeneo ya vijijini huko Kigoma kushinda.
"Naishukuru sana benki na natoa wito kwa wananchi wengine wajiunge na NBC kwani hawana upendeleo na huduma zao ni bora",alisema.
No comments:
Post a Comment