Na Karoli Vinsent
KILE kinachotafsiliwa kuwa
Demokrasia nchini imeanza kukuwa kutokana na wingi wa vyama vya kisiasa nchini
vinaanzishwa,hivi leo chama kipya cha kisiasa nchini kimeanzishwa chama hicho
kinajulika kama ACT,(Alliance for change And Transparency)maana yake ni Umoja
wa Mabadiliko na Uwazi.
Hayo,yamethibitishwa leo Jijini Dar es
Salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho kipya,Limbu Lucas Kadawi Wakati
akitambulisha Chama hicho kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo alisema
wamefikia maamuzi ya kuanzishwa chama hicho kutokana na Malengo mahususi ya
kuwaleta watu pamoja.
“Tumeanzishwa chama hichi cha
kisiasa kwa malengo mahususi ya kuwaleta
watu pamoja watanzania wanaoamini kwamba
nguvu ya Pamoja inaitajika katika kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa katika
nchi hii, na kwamba uwazi na uadilifu ni tunu ambazo taifa hili linaitajika kwa
sasa na Baadaye”alisema Limbu
Limbu alisema chama hicho cha ACT
kinatakuwa kinaongozwa na misingi mikuu mitano ambayo ndio itakuwa nembo ya
chama hicho.
“ACT tutakuwa na inaongozwa
na misingi mikuu mitano ambayo ni Uzalendo,Usawa,Uadilifu Uwazi na uwajibikaji pamoja
na Demokrasia ya Kweli”Alizidi kuongezea Limbu.
Limbu ikumbukwe Mwaka 2010 alikuwa Mwanachama
wa cha Wananchi CUF na aligombania Ubunge kupitia Chama hicho kwenye Jimbo la
Temeke na Alibwagwa kwenye uchaguzi huo na Mbunge wa CCM kupitia Temeke, Mr
Mtevu na Baada ya Hapo na kwenda kuanzishwa chama cha ADC kabla ya kuanzishwa
chama hichi.Aliwataka wananchi wakiamini chama hicho kuwa ni Chama
kitakachowaletea maendeleo .
Kwa upande wake Katibu mkuu Taifa wa
Chama hicho Samsoni Mwigamba alisema Chama hicho kwa sasa kimeanda mipango
mikubwa ya kuhakikishwa kinashinda kwenye Chaguzi Mbalimbali Zinazokuja.
“Kwa sasa ACT Tanzania imekwisha
Kukamilisha Rasimu ya awali ya Katiba ambaye iliwezesha kupata usajili wa Muda
na Zoezi la kuandikishwa wananchama katika mikoa kwa ajali ya kuomba usajili wa
kudumu kwa mujibu wa sheria limekwisha kamilika”
“Tumewapata Wanachama katika mikoa
yote ya Tanzania Bara,hata ivyo tumechagua mikoa kumi ambayo tungependa Msajili
akahakiki kama sheria inavyotaka”alisema Mwigamaba.
Ikumbukwe Samsoni Mwigamba kabla ya
kujiunga na chama hichi cha ACT alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA Mkoani Arusha na pia alikuwa mhasibu Mkuu wa Chama hicho na
Baada ya hapo Chama chake cha Chadema kilimvua uwanachama kwa kile chama hicho
kinadai kuwa Mwigamba alikuwa anafanya Uasi katika chama hicho, ambapo Kamati
kuu ilimvua uwanachama pamoja na Wananchama wengine akiwemo Ziito Kabwe pamoja
na Dk Kitara Mkumbo.
Wachambuzi wa Masuala ya Kisiasa
waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu walisema chama hicho kipya cha
kisiasa nchini uwenda kikawa kimeanzishwa kwa mahususi ya kuwachukua wanachama
waliokuwa wamevuliwa uwanachama kwenye vyama tofauti vya kisiasa nchini,huku
wachambuzi hao wakihoji kwanini chama hicho cha kisiasa kimeanzishwa
sasa,wakati vyama vya kisiasa nchini
vikiwa katika hali ya sitofamu.
Ambapo Kauli hiyo ilipingwa
vikali na Mwenyekiti wa Chama hicho cha ACT alisema chama hicho wala hakina
uhusiano wowote na Mtu wala mikoa bali chama hicho kinawahusishwa watanzania
wote.
No comments:
Post a Comment