Bidhaa ambazo huwa unazipata ndani ya soko la kariakoo sasa zinapatikana ndani ya ufukwe wa coco beach kwa gharama nafuu sana na bidhaa nzuri kwa utulivu kabisa |
wauzaji wa bidhaa hizo wakiwa wanaweka mambo sawa asubuhi hii wakati wakijiandaa kuwahudumia mamia ya wateja wa dar es salaam watakaojaa muda sio mrefu ndani ya coco beach |
Maonyesho hayo yameanza jana jumamosi na yatamalizika leo jumapili huku yakiwajia tena wikiend nyingine ya mwisho wa mwezi |
Ukifika eneo hili burudani za music mchanganyiko pia zipo kwa wingi sana |
Mabanda mbali mbali ya wafanyabiashara yakiwa tayari kabisa kama yalivyonaswa na mwandishi wa mtandao huu mapema asubuhi ya jumapili ya leo |
Muonekano wa maonyesho hayo kwa nje |
Wakina dada bidhaa zenu zinapatikana usikose |
No comments:
Post a Comment