Wednesday, March 12, 2014

HAYA NDIO MAPINDUZI YA TELEVISION TANZANIA,TV MPYA YAZINDULIWA DAR MUDA HUU NI TV ONE


Mkurugenzi wa TV1Marcus Adolfsson

Na Karoli Vinsent
      
      MAPINDUZI ya Runinga yamekuja hapa nchini,Baada leo  kuzinduliwa kituo kipya cha runinga kinachoitwa  TV1,ambacho kimesheheni vipindi bomba vya runinga vitakavyukufanya ufurahie na kutabasamu siku nzima.
      
       Hayo yametokea  leo Jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa TV1 Marcus Adolfsson wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo alisema televisheni hiyo imekuja kumaliza kiu ya Watanzania katika sekta ya habari na Burudani.


      “Hii itakuwa  ni kituo Pekee cha Runinga kitakachomaliza kiu ya kukosa vipindi bora kwa mda mrefu,kutokana na kuandaa Taarifa za Habari makini na Vipindi bora vya Majadiliano Pamoja na Tamthiliya Bomba za ndani na nchi”

        “Nataka niwatoe hofu watanzania tuko makini na tunauzoefu kiufanyaji kazi kwenye upande Runinga  na uzoefu huu ndio unatufanye tujivunie kuwa na vipindi bomba na Makini”alisema Adolfsson

Katika hatu nyingine,mtangazaji wa Taarifa ya Habari katika tv hiyo,Mershaki Zoha alisema wamejipanga vya kutosha katika upande wa Habari na habari itakuwa tofauti na Habari zingine hapa nchini, itakuwa  kitafiti zaidi.

“Na tumekuja kubadilisha sura ya taarifa ya Habari hapa nchini na kuondoa  ile tamaduni ya waliokuwa nao waandishi wengi hapa nchini kufanya taarifa zisizo za uchunguzi na kuwasemea watu,sisi tutakuwa tunafanya  habari za utafiti na kuwashirikisha wananchi kwa kiasi kikubwa”alisem Zoha.

Ikumbukwe ujio wa TV1 ni njia pekee ya kukuza sekta ya Habari na kutoa ajira hapa nchini na Kituo hicho cha TV1 kinapatikana kwenye kingamuzi cha Startimes pekee kwenye chanel namba 103.
     Kituo hicho kinamilikiwa na watu kutona Dermark na huo ni mwendelezo wawekezaji hao katika kusambaza huduma hiyo ya runinga na sasa wako njiani kwenda nchini Kenya.


No comments: