Mchungaji wa kanisa la Pentekoste William Mwamalanga akizungumza na wnahabari leo katika ukumbi wa habari maelezo juu ya mambo yanayoendelea katika taifa la tanzania |
Na Karoli Vinsent
HOFU ya Uvunjifu wa Amani kutokana mchakato wa katiba
mpya,imeanza kuwajia Viongozi wa Dini hapa nchini.
Hofu,hiyo iliibuliwa Leo Jijini
Dar es Salaam na Mchungaji wa kanisa la Pentekoste William Mwamalanga Wakati wa
mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam,ambapo alisema Kanisa la
Kipentekoste nchini limeanza kupata wasisi kutokana na mwenendo wa Bunge la
katiba hivi sasa.
“Iko dalili kubwa la Taifa letu Amani yake ikatoweka kutokana na
mchakato wa katiba mpya,naiomba serikali iwe macho katika mchakato
huu wa katiba ili yasiweze kutokea kama yaliyotokea nchini Kenya”
“Wenyewe tulikuwa Mashahidi tuliona
jinsi Mchakato wa katiba mpya ulivyomaliza watu nchini Kenya,na kuleta mahafa
makubwa watu kufa na wengine kukosa makazi”alisema Mchungaji Mwamalanga.
Mchungaji Mwamalanga,alizidi kusema
Taifa lipo katika kipindi kigumu sana kuliko vipindi vyote kutokana na macho ya
Watanzania wote kuelekezea macho yao Bungeni Dodoma katika mchakato huu wa
Katiba na akawataka wajumbe wae makini na watoe tofauti zao za kisiasa na
waweke maslai mbele ya Taifa kwani wasipofanya hivyo amani ya nchi iko Rehani
kutoweka.
Katika hatua nyingine Mchungaji huyo
alivipongeza Vyombo vya Habari kwa Kazi kubwa inayofanya kukosoa na Kuelimisha
jamii,Kauli ya mchungaji Mwamalanga imekuja siku chache Baada ya Mtandao huu
kuripoti juu Viongozi wa Dini kuanza kujiingiza katika misimamo ya vyama vya
Kisiasa na kuacha kazi yao kubwa ya kiroho.
Mtandao huu umebaini na
kutaharifu kuwa kauli aliyoitoa Askofu wa Kanisa Katoliki nchini Muadhama
Policapy Kardinali Pengo na
Tume ya Haki na Amani ya
Barazala maaskofu wa Kanisa katoliki Tanzania(TEC) umeonyesha wazi sasa kanisa
hilo kubwa hapa nchini limeanza kulipasua kanisa hilo na kuwaacha waumini wake
wakiwa njia panda,na hawajui wapi waende,kutokana na mikingano ya viongozi wao
wa dini.
Wachambuzi mbalimbali waliozungumza na
Mwandishi wa Mtandao huu wanasema mgongano huo unaojitokeza kwenye kanisa hilo
ni wazi sasa watumishi wa kiroho wanaanza kujiingiza kwenye siasa huku wakiicha
kazi yao kubwa ya imani,huku wengie wakisema kwanini Askofu pengo hawe tofauti
na wenzake wa TEC wakati wao ni wamoja na mtengano huo unaweza kuonyesha sasa
wazi kuna watu wanatumiwa na wanasiasa katika kanisa hilo.
Wachambuzi hao wakaenda mbali na kusema
TEC basi wasingeutoa hilo tamko, kwani inaonekana limetolewa bila ya
kuwashirikisha Maaskofu wenzake ,kama Wao wanasema serikali tatu inakuwaje
Askofu Pengo mkubwa kama huyo anakuwa tofauti?au wakati wanapitisha hilo tamko
walikuwa watu wachache na sio jumiya nzima ya TEC?
Habari ambazo mwandishi wa Mtandao huu
amezipata kutoka kwa waumini wa makanisa katoliki hapa nchini waliokuwa wazi
kuzunguma na mwandishi wa mtandao huku wakitaka majina yao yasitajwe
mtandaoni,walisema
Wanashangaa kwanini viongozi wao
wanakuwa wanatofautiana katika maamuzi,na kushangaa kwanini wanaingia kwenye
siasa huku wakijua siasa ni vitu vya uongo kwani bibilia imekataa viongozi wa
dini kuwa kwenye siasa,
No comments:
Post a Comment