Chama cha Alliance For Change and
Transparency Mkoa wa Kigoma,kimeshusha Bendera ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA tawi la Ujiji stendi ya zamani na kupandisha bendera ya
(ACT) wakati wa uzinduzi rasmi wa matawi sita katika manispaa ya kigoma ujiji.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo,
Katibu wa ACT Mkoa Athuman Kabogo alidai lengo la kushusha bendera hiyo ni
hatua ya kukataa kugeuzwa kuwa vibaraka wa watu wengine kwa kukosa haki ya
kuhoji na kuwania nyadhifa za chama hicho na
hivyo kuanzisha ACT kama chama cha wanyonge kinachoweza kuwasikiliza na kutoa haki kwa kila mmoja
hivyo kuanzisha ACT kama chama cha wanyonge kinachoweza kuwasikiliza na kutoa haki kwa kila mmoja
Kabogo aliwataka wanachama
wahitaji, wachukue kadi za ACT ili chama kipate usajili kamili kwa mujibu wa
sheria,kanuni na taratibu husika pamoja na kutoa michango endelevu ,ikiwa ni
jitihada za makusudi kuhakikisha chama kinasonga mbele
kwa maslahi ya Taifa.
kwa maslahi ya Taifa.
“Wananchi nyie ni chachu ya chama
kuwepo kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za mitaa kwa
kukiamini na kukipatia ridhaa kiweze kuleta
mabadiliko ya kimaendeleo” alisema Juma Ramadhan aliyekuwa katibu kampeni wa CUF kigoma.
mabadiliko ya kimaendeleo” alisema Juma Ramadhan aliyekuwa katibu kampeni wa CUF kigoma.
Kwa upande wa Katibu ACT Kanda
Magharibi Wiston Moga alisema, lengo la chama ni kuleta mabadiliko kwenye
ulingo wa siasa,ambapo wao wamedhamiria kutetea maslahi ya umma kwa lengo
la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambayo ni chachu ya vyama vya siasa
kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
Katika ziara hiyo ya uzinduzi wa
matawi ya chama husika,ACT kimefanikiwa kufungua matawi kwenye kata sita kati
ya kata 19 zilizopo katika manispaa ya kigoma ujiji,huku baadhi ya viongozi
kutoka UPD,CHADEMA na CUF wakijiunga na chama hicho
kwa kudai wanahitaji chama chenye uchungu na kukabiliana na changamoto za wanyonge.
kwa kudai wanahitaji chama chenye uchungu na kukabiliana na changamoto za wanyonge.
Hata hivyo wanachama 3500 wa chama cha
Democrasia na Maendeleo Chadema katika tawi la Ujiji mkoani Kigoma wamehamia
chama kipya cha Alliance For Change and Transparency (ACT).
No comments:
Post a Comment