Kufuatia
kile kilicho kuwa kikisubiriwa kwa hamu na watanzania wengi Kutoka Bungeni
mjini Dodoma katika Suala la Uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa Bunge maalum
la Katiba Hatimaye Mh.Samweli sitta ameweza kuibuka Kidedea muda huu Bungeni
Mjini Dodoma Baaada ya Kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti Halali wa Bunge Hilo la
Katiba.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jioni hii mjini Dodoma wajumbe wa bunge
maalum la katiba wamemchagua Bwana Samuel Sitta mjumbe kutoka chama cha
mapinduzi CCM, kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge hilo baada ya kumshinda
mgombea mwenzake, Hashim Rungwe aliyetokea chama cha NCCR MAGEUZI.
Samuel Sitta amechaguliwa kwa kupata ushindi wa kura 487 dhidi ya
mgombea mwenzake Hashim Rungwe aliyepata kura 69 kutokana na kura 563 za
wajumbe wa bunge hilo waliopiga kura na hatimaye kutangazwa na msimamizi wa
kura hizo
Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge maalum la Katiba pamoja na majukumu
mengine atakuwa na kazi ya Kuongoza mikutano na vikao vya bunge maalum la
katiba, kuongoza mwenendo wa utaratibu wa majadiliano katika vikao vya bunge
hilo na kutoa uamuzi kuhusu masuala yote ya taratibu kwa kusimamia amani na
utulivu katika vikao vya bunge
Aidha
Mwenyekiti wa Kudumu wa bunge maalum la katiba atakuwa na madaraka ya kutafirsi
kanuni ambazo wamezipitisha na uamuzi wake utakuwa ni wa mwisho, isipokuwa
katika kutekeleza majukumu yake ataongozwa na sheria na kanuni walizozipitisha
na pale ambapo kanuni hazikutoa mwongozo ataongozwa na kanuni nyingine za nchi
pamoja na mila na desturi za nchi..
Samuel Sitta ambaye pia ni Waziri wa sasa wa
Afrika Mashariki amewahi kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika bunge la tisa kipindi cha awamu ya kwanza ya awamu ya nne ya uongozi wa
Rais Jakaya Kikwete na ameondoka na historia ya kufanyika mageuzi makubwa ndani
ya bunge wakati wa uongozi wake kwa mijadala ya wazi kwa wabunge wa pande zote
kwa falsafa aliyojiwekea ya viwango na spidi, ambayo pia ameingia nayo katika
kuwania uenyekiti wa kudumu wa bunge hili la katiba. Ana taalum ya sheria.
Hashm Rungwe naye amewahi kuteuliwa na chama chake na kugombea Urais wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, naye pia ni
mwanasheria
No comments:
Post a Comment