Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Machi 30 mwaka huu) Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam imeingiza sh. 26,455,000.
Watazamaji 4,741 walikata tiketi
kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawanyo kwa mapato ulikuwa Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47, gharama za kuchapa tiketi sh.
3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh. 5,460,687.63.
Uwanja sh. 2,776,620.83, gharama za
mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh. 1,665,972.50, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.
No comments:
Post a Comment