Makamu
mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dr. Ali
Mohamed Shein akiongoza kikao maalum cha kamati Kuu ya CCM
kilichomjadili ili kumpitisha mgombea Uchaguzi kwa tiketi ya CCM jimbo
la Chalinze Bwana Ridhiwani Kikwete.Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete alitoka nje kwa mujibu wa kanuni za CCM wakati wa kikao
hicho kwasababu ana uhusiano wa moja kwa moja na mgombea.Bwana Ridhiwani
Kikwete alishinda kura za maoni wiki iliyopita na hivyo kumpa nafasi ya
kupeperusha bendera ya CCM kwenye kinyang’anyiro hicho kufuatia kifo
cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Chalinze Marehemu Saidi
Bwanamdogo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu
Abdulrahman Kinana.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu ya CCM wakiwa katika kikao maalum mjini Dodoma leo
No comments:
Post a Comment