Na Karoli Vinsent
DIBWI la kufa Mashirika
ya Umma na Viwanda limezidi kuiandama Serikali,hivi leo Ushirika wa KCU (1980)
Ltd,uko taabani mda wowote Ushirika huo utakufa,kutokana na Ufisadi unaofanywa
na Viongozi wa ushirika huo,Habari24 imebaini.
Wakulima wanaounda ushirika wa KCU (1980) Ldt.mkoani kagera
wameamua kupigia kelele bila kuchoka,hata kwa kelele hizo hazionekani
kusikilizwa na yeyote kati ya wale waliolengwa kuzisikiliza.
Habari za kuaminika ambazo mwandishi wa mtandao huu amezipa
na kuthibitishwa Wanaushirika wanaounda ushirika huo,Zinasema kwasasa
ushirika huo upo mbioni kufa kutokana na ufujaji wa pesa unaofanywa na Viongozi
wa Ushirika huo,
Wanaushirika hao wanasema kwamba kwa sasa ushirika wao hauna
chochote cha kujivunia,kitu kinachofanya ushirika wao uonekane kama mkusanyiko
au umoja wa Mateso tu.
Wanaushirika hao wanazidikusema kahawa hainunuliwi tena KCU
(1980) Ltd.kwa sasa kwa madai ya ushirika huo kutokuwa na pesa,
Wakati ikisemekana kwamba ushirika huo hauna fedha cha
kununulia kahawa,chama chao hicho kinayo madeni yasiyosemekana,pamoja na chama
hicho kuwa na vitega uchumi lukuki lakini kinachozalishwa na vitegauchumi
hivyo havionekani.
Habari ambazo mwandishi mtandao huu amepenyezewa na Wakulima
wa Ushirika huo zinasema licha ya kuwa na ukata wa pesa ushirika huo,lakini kwa
viongozi wa ushirika huo kwao ni neema tu.
Kwamba viongozi wa KCU (1980) Ldt.ni watu wanaopendelea
kujiweka ngazi moja na watu wanaoendesha taasisi zenye ukwasi wa hali ya
juu sana
Taarifa hiyo inasema hivi karibuni viongozi wa ushirika huo
waliaandaa safari ya kwenda Burundi ,safari hiyo iligarimu si chini
milioni 23,tena pesa hizo ni za mkopo toka benki ya CRDB,
Safari,hiyo haikuwa na umuhimu wowote kama
viongozi hao kutokana na hali ya ushirika huo ilivyokuwa
mbaya,kwasababu tayali ushirika huo ulikuwa na mwakilishi kule Burundi
kwa ajili ya matakwa ya kitaalamu.
Hatahivyo inasemekana wajumbe wengine ya bodi walienda kutalii
tu ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuongezea mzigo KCU ,bila ya sababu yeyote,
Taarifa za kuaminika zinasema baada ya ujumbe huo kutoka
kwenye safari hiyo ya kitalii nchini Burundi inadaiwa kuwa vilianza vikao vya
siri kutaka kujua ni mtu gani anatoa nje siri za viongozi,
Wakilima wengi wa kahawa wa mkoa wa Kagera, hususani walio chini ya chama kikuu cha ushirika cha KCU (1990) Ltd., wamezoea kuuza kahawa yao kupitia vyama vyao vya msingi kwa kutegemea bei wanayopangiwa na wanunuzi. Mnunuzi mkuu wa kahawa yao ni chama chao kikuu cha ushirika, KCU (1990) Ltd..
Chama hicho ndicho kinachowapangia bei wakulima kulingana na
uongozi wake unavyojisikia.Ushirika huo kwa sasa huko katika hali mbaya
kutokana na ufisadi mkubwa ambao unaofanywa na wajumbe wa bodi hiyo.
Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta waziri wa Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza,kutaka kujua kwanini
serikali inawafumbia macho viongozi hao wa KCU Ltd ambao wamekuwa wakifanya
ufisadi,Simu ya Waziri huyo iliita bila ya kupokelewa.
No comments:
Post a Comment