Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
Kufuatia makubaliano hayo TFF tulipatiwa vifaa
kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars). Vifaa
hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya
Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na
Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni
washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka
mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.
No comments:
Post a Comment