TAIFA STARS KUREJEA JIONI KUTOKA NAMIBIA
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kurejea nchini kesho (Machi 7
mwaka huu) kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya
FIFA.
Taifa
Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare
ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.00 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
Timu
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli
ya Accomondia kwa ajili ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi
yake.
No comments:
Post a Comment