Wednesday, April 16, 2014

EXCLUSIVE---HII NDIO STORY YA JARIBIO LA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII LA KUTAKA KUIFISIDI NCHI NA KUZIMWA NA IKULU.SOMA



Na Karoli Vinsent

JARIBIO la Ufisadi lilokuwa linaratibiwa na Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu,la kuuza Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa kampuni ya Africa Parks Networks (APN) la nchini Afrika kusini,Sasa limeota mbawa.

Hii imekuja baada vyombo mbalimbali vya Habari,ikiwemo mtandao kuibua Tuhuma hizo za Kifisadi.

Taarifa za kuaminika ambazo mwandishi makini wa mtandao huu amezipata zinasema,jaribio hilo la kifisadi limeota mbawa kutokana na Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kugundua njama hizo.


Chanzo hicho kilizidi kusema mpango huo wa kifisadi ulikuwa umesukwa na Waziri huyo na Mbunge wa Kahama,Jemes Lembeli,ambaye inasemekana ni mwenyekiti wa Bodi kampuni ya APN.

Taarifa hiyo ilizidi kufafanua kuwa mpango wa kutaka kupora maeneo ya Wanyama pori ambayo yako kisheria hapa nchini sio geni,kwani jaribio hilo limekuwa likitaka kufanyika tangu mwaka 2012.

Chanzo hicho kilizidi kusema shinikizo la Lembeli kutaka makabulu hawo wapewe Hifadhi,alijiigemeza kwenye madai kuwa serikali imeshindwa kulinda wanyama pori                     kutokana na kuwepo ongezeko la ujangili.

Vilevile chanzo hicho kilihoji uhusiano wa karibu kati ya Waziri Nyalandu na Mbunge wa Kahama Jemes Lembeli,wakati ikisitishwa kwa oparesheni tokomeza ujangili kulikofuatiwa na hatua bunge kutaka kamati ya bunge ya Ardhi,Maliasili na mazingira inayoongozwa na Lembeli kuchunguza mwenendo wa Oparesheni hiyo.

Ndipo kamati hiyo ilonyesha udhaifu mkubwa kwa mkurugenzi wanyama pori,ambaye inasemekana  ni kikwazo kwa Lembeli katika kufanikisha mradi wake huu wakuuza Hifadhi.

Ikumbukwe Ripoti ya Lembeli ndiyo iliyofanikisha Balozi Khamisi Kagasheki kujiuzulu uwaziri wa maliasili na utalii,katika hali iliyowashangazawengi Waziri wa sasa wa Wizara hiyo malakwamala amekuwa akiibeza Ripoti hiyo na kusema imejaa uwongo na upotoshaji mkubwa.

Kauli hiyo ya Nyalandu ilizidi kuwaudhi Viongozi wa Kamati hiyo na kumfanya Mwenyekiti wa kamati hiyo Jemes Lembeli kutaka bunge limchukulie hatua za Kinidhamu kutokana na Kauli yake hiyo.

Katika hali ya kushangaza Licha ya kuwa na Uadui mkubwa sana Kati ya Nyalandu na Lembeli,baada ya kupata uwaziri wa Maliasili na Utalii tu,ukaibuka urafiki wa karibu kati ya Waziri huyo na Lembeli,ambalo ulianza kuwatia shaka watumishi wa Wizara hiyo.

Chanzo hicho kilizidi kusema Waziri Nyalandu alitumia Ndege ya Idara ya Wanyama Pori January 18 mwaka huu na kumfuata Lembeli kahama na baadaye walionekana wakiwa kwenye chuo cha Taaluma ya Wanyamapori,pasiasi Jijini Mwanza.

Huku Nyalandu na kusema hana Tofauti Yeyote na lembeli,huku naye lembeli akisema hana tofauti Yeyote na na Waziri huyo huku wengine wakihoji urafiki huo wa karibu kati ya Nyalandu na Lembeli umechagizwa na nini?ni wazi waziri Nyalandu alisharidhia kuuza hifadhi hiyo na Lembeli.

Duru hizo zilisema Ridhaa ya Nyalandu kuuza mbuga zetu zilianzapale alipokubali wazo la Lembeli la kumngoa Mkurugenzi wa Wanyama Pori,Profesa Alexander Songorwa,huku Lembeli akijua wazi Nyalandu kavunja Sheria za utumishi wa Umma.

Licha ya wataalamu mbalimbali kuonyesha hatali kubwa kwa Siasa kuingizwa kwenye masuala ya Hifadi huku wakitoa mfano kwenye kadhaa ikiwemo Malawi,Rwanda,zambia,kongo,lakini waziri Nyalandu alipuuzia ushauri huo.

Chanzo hicho kilizidi kusema wakati akiwa uwanja wa Ndege wa mwalimu Juliasi Nyerere (JNIA) na wenzake wakiwa wanataka kusafili kwenda Afrika ya kusini alionyeshwa gazeti moja la wiki,ambalo liliandika habari ya Nyalandu auza hifadhi ya Katavi.

Ndipo Gafla akapigiwa simu na kutakiwa kuripoti ikulu haraka sana,huku Nyalandu akawaacha wenzake waendelee na safari yeye alirudi na kwenda ikulu.

Licha,ya Waziri Nyalandu kujitetea kuhusu Safari hiyo,lakini ikulu ilimtaka na kusema Suala la Ikulu halina Mjadala,ingawa haikujulikana alichoitiwa ikulu,lakini wadadisi wa mambo wanasema uwenda ilikuwa suala hili la ubinafsishaji wa Hifadhi,

Baada,ya kuachwa na Ndege lakini waziri Nyalandu bado alionekana yuko makini katika kufanikisha Nia yake ya kuuza Hifadhi hiyo,aliondoka na Gari na Kwenda Arusha na baadaye kwenda Nchini Kenya na kupanda Ndege ya shirika la Kenya na kwenda kuungana na wenzake ili kuwai mkutano na Kampuni ya APN .

Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta Waziri nyalandu ili azungumze Juu ya Tuhuma hizi Simu yake haikuweza kupokelewa.

Jitihada,za Mwandishi wa Mtandao huu kutaka kujua ukweli alimtafuta Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mchungaji Piter Msigwa ambapo alisema wao nao wanafuatilia Suala hilo na watalitolea ufafanuni juu ya Tuhuma hizo.


No comments: