Katibu Mtendaji wa NACTE Dokta Primus D Nkwera akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam |
Na Karoli Vinsent
BARAZA la Vyuo vya Ufundi
nchini(NACTE) limesema Tatizo la Vyuo Feki halitakwisha Tanzania, kutokana na
Vyombo vya Habari nchini kuhusika katika kuvitangaza vyuo hivyo.
Hayo yalisemwa leo na Katibu
Mtendaji wa NACTE Dokta Primus D Nkwera wakati wa mkutano na Waandishi Habari
makao makuu baraza hilo jijini dar es Salaam,ambapo alisema tatizo la vyuo feki
ambavyo havijasajiliwa havitakwisha kutokana na Vyombo vya Habari nchini kuzidi
kuvitangaza.
“Mimi nataka nikwambia tatizo hili
la vyuo feki halitakwisha hapa nchini kutokana na vyombo vya Habari kuzidi
kuvitanga vyuo hivi,leo ukiangalia kwenye television utaona kati ya matangazo
nane ya vyuo yanoyotangazwa,kati ya hivyo vyuo vinne havijasajiliwa”alisema
Nkwera
Nkwera alizidi kusema wao walishakaa
na Wahariri wa vyombo hivi vya Habari kuhusu kuvibana vyuo hivi.
“Tulishakaa na wahariri wa vyombo
mbalimbali vya Habari tuliambiwa eti suala hilo la watu wa masoko ndio
wanahusika kwahiyo wao hayawahusu tena, huku wengine wakisema hawezi kufanya
hivyo ”aliongeza Nkwera
Hata Hivyo vyote ambavyo vitataka
kuchukua wanafunzi wanoanza shahada ya cheti wanatakiwa kumchukua mwanafunzi
aliyepata D mbili na E tatu ndiyo wanatakiwa kutumia badala ya mfumo wa Zamani
wa D tatu.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kutoka wizara wa Afya Dr Otilia Gowelee |
Katika hatua nyingine Baraza hilo
limewataka wanafunzi wote wanaotaka kuomba mwaka wa masomo kwenye vyuo vya Afya
nchini watumie njia ya mtandao.
Akizungumzia hayo Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu kutoka wizara wa Afya Dr Otilia Gowelee alisema kwa sasa wanafunzi
wote ambao wanataka kuomba ngazi ya cheti na Diploma kwa sasa wanatakiwa kuomba
kwenye mtandao.
“Tunawaomba wanafunzi wote wanaotaka
kuomba ngazi ya cheti au Diploma kwenye vyuo vya afya nchini wanatakiwa kuomba
kupitia kwenye mtandao,kuliko utaratibu wa mwanzo,kwa sasa wanafunzi wanaweza
kwenda kwenye mtandao wa NACTE,nakuanza kuomba”alisema Gowele
Gowelee aliitaja miatandao ambayo
wanatakiwa kutumia kuomba ambayo ni, www.nacte.go.tz, au www.moh.go.tz,
www.cas.ac.tz
Ikumbukwe kwa sasa Baraza hilo
limevisajili vyuo 11 kwa mda wa wiki moja,na kwa sasa baraza hilo
limewataka watu wote wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kuanza kuomba kwa sasa
maana Nafasi zimefunguliwa ziko wazi cha msingi uwe umefahulu kwa kiwango
kizuri na mwisho wa kuomba nafasi hiyo ni 30 mwezi wa Sita
No comments:
Post a Comment