Msemaji wa taasisi za Kiislaam Tanzania RAJABU KATIMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam |
Na Karoli Vinsent
KAULI ya uchochezi na kuligawa Taifa
kidini aliyoitoa kanisa, Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu(sera,uratibu
na Bunge) William Lukuvi.Sasa Yazidi kuibuwa Makubwa.
Hivi leo Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu nchini, wameandaa kongamano kubwa ili kumshinikiza, Rais Jakaya
Kikwete amfukuze kazi,Waziri Lukuvi katika nafasi hiyo,kwa kile wanachokidai
analigawa Taifa kidini na kuleta machafuko.
Hayo yalisemwa Leo, na Msemaji wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Rajabu Katimba wakati wa mkutano na
Waandishi wa Habari,ambapo alisema wamefikia maamuzi hayo kuandaa kongamano
hilo kutokana na kauli ya kichochezi aliyoitoa waziri huyo.
“Sisi hatukutalajia Waziri mwenye
mamlaka makubwa na aliyeaminiwa na Rais na kumwakilisha waziri mkuu kutamka
kauli chafu na za uchochezi tena kanisani dhidi ya waislamu nataasisi ya
kiislamu iliyosajiliwa kihalali”
“kauli hizi zina nia ya kuletea
chuki,kuwatia woga wananchi na hatimaye kuchafua Amani ya nchi na Tumeandaa
kuongamano hili kumshinikiza Rais amwajibishe waziri Lukuvi”Alisema
Katimba
Katimba,alizidi kusema wao
wanashangaa kimya cha Serikali kumwacha waziri huyo akifanya uchochezi na
kuligawa taifa.
“Tunashangaa mpaka sasa viongozi wa
Serikali wamekaa kimya na kumwacha Waziri lukuvi akifanya uchochezi,Je maneno
yaliyotamkwa na Sheikh Ponda kuhusu mfumo wa Kristo dhidi ya Waislam
yanalingana na haya mh Lukuvi ya chuki na uchochezi”
“Kwa mwenendo huo wa Mh Lukuvi,kwa
nini Waislamu na wapenda Amani wote tusiamini kuwa kuna mpango wa Siri
kuongamiza Viongozi wa Kiislamu na kuhalalisha mauaji hayo kwa Propaganda na
Uchochezi wa Mh Lukuvi?”alihoji Katimba
Kitimba,aliwataka viongozi wa Dini
zote kuungana na Kujitokeza kwenye Kongamano la Amani la litakalofanyika tarehe
27 mwezi huu kwenye Makao makuu ya Taasisi hiyo iliyopo Kinondoni Jijini Dar Es
Salaam ili Kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete amwajibishe Waziri Lukuvi,na
Kujadiri hatma ya Katiba.
Ikumbukwe kauli hiyo ya uchochezi
aliitoa Waziri Lukuvi alipokuwa anamwakilisha Waziri Mkuu,kwenye kanisa la
Methodist jimbo la Dodomo wakati wa Sherehe za kumtawaza mchungaji Joseph
Bundala kuwa Askofu,ambapo Waziri lukuvi alitamka wazi wazi kwamba Serikali
Tatu zikipita eti nchi haitotawalika na kuchukiliwa na Jeshi na vilevile
makanisa yote nchini yatafungwa na kwamba nchi itakosa Amani.
Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM,alizidi kuongeza kwamba Wanzazibari wanataka kujitenga hili kujitangazia
nchi ya Kiislam.
No comments:
Post a Comment