SIRI ya Serikali kuzima maandamano
pamoja Mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)Nchi nzima,HABARI24
imedokezwa siri hiyo.
Sababu hiyo ni ya kuwakataza UKAWA
kufanya mikutano nchi nzima mpaka sherehe za Muungano zitakazomalizika,ambapo
sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii
Chanzo hicho kilisema Sababu ya Serikali
pamoja na Chama cha Mapinduzi CCM,kufanya hivyo inalengo ya kumpa nafasi Rais
wa Tanzania Bara Jakaya Kikwete,ambaye anatarajiwa kutoa hutuba katika
Sherehe hizo, na vilevile itawafanya UKAWA kukosa nguvu kwa Wananchi.
“Ujue serikali inaakiri sana ndio maana
tumekataza mikutano yote ya hawa Jamaa UKAWA nchi nzima ili mpaka Rais atakapo
toa hutuba kali sana, ambayo itawafanya umoja huo ukose Hoja ya kuwadanganya
wananchi,kwani Serikali ikiwaachia Hawa wajamaa waanze kupita nchi nzima Harafu
Rais Kikwete aje kutoa hutuba,itakuwa haina maana”kilisema Chanzo hicho
Umoja ,huo wa Katiba ya Wananchi ambao
ulitakiwa kufanya Mikutano pamoja na Maandamano Nchi nzima yenye Lengo ya
kuwaelimisha Wananchii Juu ya kile wananchokiita ni kukataliwa Rasimu ya
pili Buge Maalum la Katiba.
Vilevile Sababu nyingine ya Umoja
kuwaeleza Wananchi juu Kauli ambayo ya Kichochezi na kuligawa Taifa
kidini aliyoitoa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Bunge), William Lukuvi alipokuwa kanisani mjini Dodoma .
Chanzo hicho kizidi kusema Rais
Kikwete ameshtushwa sana na Kufadhaika kutokana na hatua waliofanya UKAWA
ambayo ilimpa wakati mgumu sana kushindwa cha kufanya.
“Kwa hatua hii waliofanya hawa
watu,Rais amekosa njia ya kufanya Badala yake ameamua kuwaambia Ukweli wananchi
katika, siku hiyo ya Sherehe za Muungano ili Umma uamue wenyewe juu hali iliyopo”
“Ukiangalia mwenyewe sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya 2011 pamoja na marekebisho yake ya 2012 na 2013
inawataja Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi kuwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kwa mujibu wa
nafasi zao”.
“Kadhalika sheria hiyo inampa Rais
mamlaka ya kufanya uteuzi wa wajumbe 201 kutoka makundi mbalimbali, lakini
haitaji sifa wanazopaswa kuwa nazo wajumbe hao.
Hata kama sheria ingekuwa inaruhusu
kufukuzwa au kusitishwa kwa ujumbe wa wabunge hao, hakuna sababu ya msingi ya
kuwachukulia hatua hiyo. Na unafikili hata wewe ungekuwa Rais Kikwete
Ungefanyaje maana Sheria haikuruhusu hata kuwaengua UKAWA bungeni na kuteua
watu wengine”Kilisema Chanzo hicho Ukawa, walikawataliwa kufanya
mikutano yao na Jeshi la polisi nchini ili kupisha Sherehe za muungano.
Umoja huo
wa Ukawa unatokana muunganiko wa vyama vya CUF, Chadema, NCCR Mageuzi,
NRA, NLD na baadhi kutoka kundi la 201.am
bapo kwa kauli moja walisema
Hawatarudi tena kwenye vikao hivyo vya Bunge
No comments:
Post a Comment