Wednesday, June 18, 2014

BREAKING NEWS; RATIBA LIGI KUU ENGLAND YATOKA, MAN UNITED KUANZA NA SWANSEA, MAN CITY NA...RATIBA NZIMA IKO HAPA

KOCHA Louis van Gaal amepewa mwanzo laini katika klabu yake mpya, Manchester United baada ya kutoka kwa ratiba ya msimu ujao ya Ligi Kuu ya England 2014/2015. 

Ni tofauti na kocha aliyemtangulia, David Moyes, ambaye alipewa mwanzo mgumu msimu uliopita akirithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu.
Mwalimu huyo wa Kiholanzi, ambaye ataanza kazi Old Trafford baada ya Kombe la Dunia, amepangiwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu nyumbani dhidi ya Swansea City Agosti 16, mwaka huu.
Baada ya hapo atakwenda kucheza mechi mbili ugenini dhidi ya Sunderland na Burnley kana ya kurejea nyumbani kukipiga na Queens Park Rangers Septemba 13. 


Mwanzo laini; Kocha Louis van Gaal ataanza na mechi nyepesi Ligi Kuu England msimu ujao Manchester United 

RATIBA MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND

Arsenal v Crystal Palace
Burnley v Chelsea
Leicester City v Everton
Liverpool v Southampton
Manchester United v Swansea City
Newcastle United v Manchester City
Queens Park Rangers v Hull City
Stoke City v Aston Villa
West Bromwich Albion v Sunderland
West Ham United v Tottenham Hotspur
(Mechi zitachezwa wikiendi ya Agosti 16 na 17, mwaka huu

No comments: