Makamu mwenyekiti wa chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS FLAVIANA CHARLES akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam mapema leo juu ya kesi hiyo |
Baada
ya kesi iliyokuwa imefunguliwa katika mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya waziri
mkuu wa Tanzania MIZENGO PINDA kutupiliwa mbali na mahakama hiyo mapema wiki
jana,chama cha wanasheria Tanganyika TLS pamoja na kituo cha sheria na haki za
binadamu LHRC ambao ndio waliomshtaki
waziri mkuu leo wametoa tamko lao juu ya
kufutwa kwa kesi hiyo huku wakitangaza kurudi tena mahakamani kupinga baadhi ya
vipengele kwenye hukumu hiyo,
Wanasheria hao wakiwa wanatoa tamko lao |
Akizungumza
na wanahabari makamu mwenyekiti wa chama cha wanasheria wa Tanganyika Bi FLAVIANA CHARLES amesema kuwa kimsingi wamepokea uamuzi huo wa
mahakama na kuridhika na tafsiri ya mahakama kuhusu ibara ya 100(2) kwamba
kinga ya wabunge ina \ mipaka na ukomo
kisheria na inapashwa kuzingatia katiba na sheria nyingine nchini,hivyo kinga
hiyo inaweza kuhijojiwa mahakamani ambapo amesema kuwa hilo ni jambo muhimu
sana ambalo litasaidia kujenga misingi ya kuheshimu haki za binadamu na utawala
wa kisheria na utawala bora.
MPALE MPOKI ambaye ndiye kiongozi wa Mawakili hao waliofungua kesi hiyo |
Wakili PETER KIBATALA akizungumza na wanahabari katika mkutano huo |
Aidha wanasheria
hao wamesema kuwa hawajaridhika na kipengele kilichopo katika hukumu hiyo
ambacho kinasema kuwa kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha
Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kuwa ni mashirika na sio watu binafsi na
hawakuwa na uwezo wa wa kisheria wa kufungua shauri hilo makahakamani kwa kuwa
kauli za waziri mkuu hazingeweza kuwaadhiri wao moja kwa moja,kauli ambayo wanasheria
hao wameipInga na kuahidi kurudi mahakamani kukata rufaa juu ya kipengele hicho
na kuiomba mahakama itengue kipengele hicho.
Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC HAROLD SUNGUSIA akizungumza |
Kesi dhidi
ya waziri mkuu ilifunguliwa mnamo Augost 1 mwaka 2013 katika mahakama kuu ya Tanzania
kupinga kauli zake alizozitoa bungeni mnamo tarehe 20 mwezi wa 6,2013 alipokuwa
akijibu maswali ya papo kwa papo ambapo aliwataka polisi kuchukua hatua ya
kupiga watu endepo watafanya fujo kama tunavyoinukuu hapo chini.
“UKIFANYA FUJO, UMEAMBIWA USIFANYE HIKI UKAAMUA WEWE KUKAIDI UTAPIGWA TU,EEH MAANA HAKUNA NAMNA NYINGINE,
EEH MAANA LAZIMA TUKUBALIANE KUWA NCHI
HII TUNAIENDESHA KWA MISINGI YA KISHERIA,SASA KAMA WEWE
UMEKAIDI HUTAKI,UNAONA KWAMBA NI IMARA ZAIDI,WEWE NDIO JEURI ZAIDI,WATAKUPIGA
TU,NA MIMI NASEMA WAWAPIGE TU,KWA SABABU HAKUNA NAMNA NYINGINE,EEH MAANA TUMECHOKA SASA".
No comments:
Post a Comment