Saturday, June 14, 2014

exclusive--MBUNGE JAMES LEMBELI ALIPELEKA MAHAKAMANI GAZETI LA FAHAMU,SOMA CHANZO KIZIMA HAPA

Na Karoli Vinsent

          MBUNGE wa Kahama Jemsi Lembeli (CCM)ameanza kuweweseka kutokana na Kasfa zinamokabili na sasa ameamua rasmi kukimbilia mahakamani na kwenda kushtaki Gazeti la Fahamu pamoja na Mhariri wa Gazeti Jamhuri,mtandao huu umedokezwa

         Kukimbilia huko Mahakamani kumeibuka ikiwa ni siku chache tu kupita baada ya magazeti mbalimbali pamoja hayo na Mitandao mbalimbali yakijamii,
vikimtuhumu Mbunge huyo kwa kitendo chake cha kufanya upendeleo na kuipa tenda Kampuni ya APN  isiyokuwa na sifa za uwekezaji na kupatiwa kazi ya uwindaji kwenye Mbuga zetu hapa nchini.


          Lembeli,ambaye ni mwenyekiti wa kudumu ya Bunge kuhusu Ardhi,maliasili na Madhingira,amefungua kesi hiyo kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu,Dar es Salaam kupitia kampuni moja ya uwakili ya M/S law Bridge,kesi hiyo yenye Namba  151 ya mwaka huu(2014).

        Ambapo,anadai Makala zilizochapishwa kwenye Gazeti la Fahamu katika matoleo yake ,zimemkashifu pamoja kumdhalilishwa  kwa kumsingizia.

       Lembeli,ambaye ni Mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM,anazidi kudai Gazeti hilo linalotoka malamoja kwa Wiki,limemwalibia Hadhi yake aliyoipata kwenye Jamii,ambapo anasema anataka kulipwa Fidia kutokana na kuchafuliwa huko.

          Kwa upande wao wamiliki wa Kampuni ya FAHAMU company Limited,ambao ni wachapishaji wa Gazeti la Fahamu,katika taarifa yao ilichapishwa kwenye Gazeti hilo toleo Namba 290 la jumanne juni 16 hadi 16 mwaka huu,wameibuka na kusema wao wamezipata taarifa hizo na kusema hawataogopa.

         “Uongozi  wa Fahamu gazeti unachukulia kesi hiyo kama wasaa mzuri wa kujipima kwa Jami,kwa kazi inayofanywa na Gazeti hili ya kuelimisha jamiii kutambua haki zao”

        “Isitoshe ,ni bahati nzuri kwamba Lembeli anajulikana ,anajulikana hata alipotoka ,anajulika hata hajakuwa mbunge”
Vilevile wamiliki hao wa Kampuni hiyo ya Gazeti hilo,walizidi kusema kitendo anachokifanya cha Kimbilia Mahakamani,kinaonyesha Jinsi alivyokuwa Mbumbumbu katika kumbukumbu,kwani wanaushahidi wote.

         “Hivi Lembeli anamdanganya nan kwama ajakwenda  Afrika ya kusini kukutana na wakuu wa Kampuni ya APN?ajiandae kujitetea hoja yake kuwa hakuwamo kwenye msafala na Waziri nyalandu “
“Taarifa za kutosha zinaonyehsa kuwa msafala huo alikuwepo lembeli,uligaramiwa na Serikali na safari hiyo ilianza Machi 26 na kukamilika Machi 30 mwaka huu kutoka Tanzania kwenda Afrika ya kusini” 

         Mbunge huyo katika Kesi hiyo,anasema hajuani na Hiyo kampuni ya APN,na vilevile Lembeli akisema hajawai kwenda Afrika ya kusini kukutana na Wakurugenzi hao,

     Duru za Kisiasa zinasema kitendo cha Mbunge huyo anayeaminika kwa  Umma kukimbilia Mahakamani,
kitampunguzia sifa aliyokuwa nao,kwani vyombo vyote vya Habari haviwezi kumwandika mtu mmoja bila ushahidi,kwani hata uhusiano wake wa Gafla na Waziri wa Maliasili na Utalii lazalo Nyarandu unatia shaka,kwani watu hao wawili waliokuwa na uadui mkubwa sana hapo mwanzoni.

          Sasa kitendo cha sasa kuibuka urafiki wa karibu ni ishara kuna kitu hapo,ambacho kitakuwa kinafanyika,
Naye,msomi na Mchambuzi wa Masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma Seiph Yahaya,alisema kitendo cha Lembeli kukimbilia mahakamani ni ishara ya mbunge huyo kuanza kutapatapa.

      “Hapo,Lembeli anatapatapa tu mwandishi,kwasababu ushahidi uko wazi kabisa kwamba alikwenda kukatana na hao wakurugenzi wa kampuni hiyo ambayo ni ya kitapeli ya APN,hivi aingiii akirini mwandishi”’

“yeye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge,alafu alipiwe safari ya kazi ya bunge na Taasisi nyingine kama si kuna kitu hapo,nataka niwambie wananchi hizi ndio siasa za Majitaka za wanasiasa wetu,harafu leo anakwambia anataka kujiunga na chama cha Upinzani cha gani kitachukua watu kama hao”alisema Seph Yahaya


No comments: