Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Mosi Kimosa ,7, anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Msimba iliyoko Kigoma Vijijini na binti Trisa Luziga,6, anayesoma darasa la kwanza mara baada ya Mama Salma kutua katika uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ajili ya kumpokea Mama Salma aliyeenda mkoani huko tarehe 13.6.2014.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Issa Machibya akimpokea rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma tarehe 13.6.2014. Mama Salma yuko mkoani humo kuhudhuria maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Kigoma tarehe 14.6.2014.
Saturday, June 14, 2014
MAMA SALMA KIKWETE AWASILI KIGOMA AKIWA MGENI RASMI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA UCHANGIAJI DAMU SALAMA KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment