Mkurugenzi mkuu wa ZIFF MARTIN MHANDO akizungumza na wahabari mapema muda huu jijini dar es salaam kuhusu tamasha la ZIFF mwaka huu |
Tamasha
maarufu nchini Tanzania na Africa yote la ZIFF limezinduliwa rasmi leo jijini dare
s salaam ambapo tamasha hilo litaanza rasmi visiwani Zanzibar,kuanzia tareke 14
mwezi huu ambapo wasanii mbalimbali watahudhuria.
Kwa mujibu
wa Mkurugenzi mkuu wa ZIFF, MARTIN
MHANDO amesema kuwa takribani filamu 79 zitaonyeshwa
kwa siku kumi, katika tamasha la mwaka huu kutoka katika nchi kadhaa za Africa na
nchi za majahazi zikiongozwa na filamu kadhaa ambazo zimeshawahi kushinda tuzo katika matamasha mbalimbali
duniani,ambapo filamu za mwaka huu zinatoka katika nchi 35 ambapo 38 ni filamu fupi ,23 filamu ndefu
na 18 zitakuwa filamu za makala,
Msanii MZUNGU KICHAA naye atakuwepo huko zanzibar |
Katika tamasha hilo takribani wanafunzi 2000 watapata nafasi ya kuangalia filamu za watoto na kuzijadili katika jukwaa lao la watoto ikiwa ni sehemu ya udhamini wa shirika la save the children Zanzibar,mada kuu ya mwaka huu itahusu MAZINGIRA na kauli mbiu itakuwa MAZINGIRA SALAMA.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ONE ambaye ni mmoja kati ya wasanii watakaotoa burudani huko zanzibar |
Aaidha katika tamasha hilo wasanii mbali mbali
kutoka Tanzania na nje ya Africa watapata nafasi ya kutoa burudani wakiwemo
MZUNGU KICHAA,ONE THE INCREDEBLE,AY,SAUT SOUL NA WENGINE WENGI SANA TOKA AFRIKA
YA MAGHARIBI huku familia ya LUPITA NYONG’O ikitarajiwa kushiriki siku zote za tamasha
hilo
Wanahabari na wadau mbalimbali |
No comments:
Post a Comment