Mmoja wa Wanakamati wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo (CDF) Jimbo la Hai akipanga kuni katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Shirimatunda iliyoko wilayani Hai, wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Freeman Mbowe (Mbunge wa Hai), alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo mfuko huo utasaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Chumba hicho mbali ya kutumika na wanafunzi kwa ajili ya kusomea, pia kinatumika kama stoo ya kuni za kupikia chakula cha wanafunzi shuleni hapo, hali ambayo inadhihirisha kuwepo kwa mahitaji ya vyumba kwa ajili ya matumizi mbalimbali. |
No comments:
Post a Comment