![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7AVJsv9jI_6MjAytPFkfeBcWoCJYbVSFVKKuGIHGntQOE2KJ_e2CTk4u4JAIQ1rom-brTBP0RwI7SqblUjBtazaIL_HBxtQWc_uY_Pd_QHbGIOnePaMHTesfaRR9nZmAUUes9vKusiPc/s1600/02.jpg)
Akihutubia baada ya kukabidhiwa sime ambayo ni ishara ya kuwa kiongozi wa watu wa Malawi, Rais Mteule Mutharika alisisitiza kuwa, katika kipindi cha utawala wake atahakikisha kuwa anaifanyia makubwa Malawi sambamba na uhakikisha kuwa anaifanya Malawi itimize majukumu yake ya kimataifa kufuatia kutambua kuwa kujitenga kunaweza kuifanya Malawi kutonufaika na fursa zilizopo duniani.
“Nchi hii ipo katika dunia na siyo rahisi tena kuwa na fikra kwamba Malawi inaweza kubaki peke yake kama kisiwa. Tunahitaji kuwa na wenzetu wa kusaidia maendeleo ya Malawi. Tunawahitaji wahisani toka Kusini ama Mashariki, tunayahitaji mataifa tajiri na mataifa yanayoendelea. Tutafanikiwa sana kama tutaendeleza urafiki kwa wote. Tufanye hivi bila kujali kuwa
sisi ni taifa kwani hali ya sasa inahitaji kila mmoja wetu kushirikiana na mwenzake,” alisema.
Katika hotuba hiyo pia amesisitiza kuwa kipindi chake cha utawala atajitahidi kukabiliana na rushwa na kwamba hatakuwa na mchezo kwa wala rushwa katika kipindi akiwa madarakani. Pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuiunganisha Malawi kwa miundombinu bora ili kuboresha maisha ya wananchi sambamba na kusogeza huduma za wananchi karibu.
Rais Mutharika aliapishwa juzi baada ya kuwashinda washindani wake akiwemo Rais aliyemaliza kipindi chake Joyce Banda ambaye hata hivyo hakuweza kutokea katika sherehe hizi za kukabidhi madaraka. Akizungumzia suala la kutohudhuria kwa Rais Banda, Rais Mteule Mutharika alisema alitegemea Rais Banda kuwepo lakini hakufika nay eye anatambua kuwa wakati wa uchaguzi kulikuwa na tofauti baina yao lakini kwa sasa uchaguzi umeisha na amesahau yaliyopita ili kuanza ukurasa mpya wa kuijenga Malawi. Katika shughuli hiyo pia Rais wa zamani wa Malawi Kamuzu Banda alihudhuria.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal na msafara wake walitarajiwa kurejea nyumbani leo hii Jumatatu mara tu baada ya kukamilika kwa kazi hii ya makabidhiano.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment