Na Karoli Vinsent
KATIKA kujali ubora wa Gazeti la Mwanahalisi mtandao huu,unakuleta
simulizi kuhusu sakata la kufungiwa Gazeti hilo,ambapo gazeti hilo limefungiwa
kwa mda usiojulikana na Serikali kutokana na Habari zake zilizokuwa
zikiandikwa.
Gazeti
la mwanahalisi lilifungiwa Tarehe 30/07/2012 na Waziri wa Habari ,vijana utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ambapo
alitoa Hukumu ya kulifungia kwa muda usiojulikana kwa kile alichokiita kwamba
mwenendo wa Gazeti hilo si mzuri,kwani limekuwa likiandika Makala zenye
uchochezi na kuleta Uhasama na
uzushi na kupelekea wananchi kukosa Imani na Vyombo vya Dola hali inayoweza
kuhatalisha Amani ya nchi.
Ambapo, waziri huyo alitumia Sheria Kandamizi ya Magazeti ya Mwaka
1976,kifungu Namba,25 ambayo inampa Mamlaka waziri anae husika na masuala ya
Habari, kulifungia Gazeti lolote pale yeye mwenyewe anaona kwa mawazo yake
kwamba Gazeti linakiuka sheria ya nchi.
Adhabu
hiyo ilianza kutumika kwanzia Tarehe 30 mwezi Julai mwaka 2012,ambapo katika
adhabu hiyo ilisema kwanzia sasa gazeti hilo limefungiwa kwa mda usiojulikana.
Kwa
sasa Gazeti hilo limetimiza Miaka miwili tangu lifungiwe lakini bado hakuna nia
ya dhati kutoka kwa Serikali katika kulegeza Adhabu hiyo kubwa kwenye historia
ya Magazeti nchini, huku serikali ikijua kwamba Nchi yetu Tanzania iko kwenye
,Mfumo wa Kidemokrasia ambao unatoa mwanya kwa Mtu kujieleza,
Vilevile
Serikali imeshindwa hata kutambua kwamba ndani ya Katiba ya nchi Ibara ya 18 ambayo inatoa uhuru wa
kujieleza kwa kila mtu.
Mtandao
huu utakuletea Mikingano ambayo imeibuka baada ya Gazeti hilo kufungiwa kutoka
Kwa Viongozi,ambapo malamala kwa mala wamekuwa wakitofautiana kuhusu kufungiwa
gazeti hilo ambalo lilibeba Taswira ya ukombozi katika fani hii ya Habari.
Gazet la Mwanahalisi lilianzishwa miaka mitano iliyopita na kuwa chini ya
Kampuni ya Halihalisi Publishers Ltd,ambapo mkurugenzi wa Kampuni hiyo alikuwa
ni Said Kubenea.
Vilevile Kubenea ambaye ni miongoni mwa Waandishi bora wanofanya Habari
za uchunguzi nchini,ambaye alikuwa anafuata nyayo za Mwandishi wa Zamani Gazeti
la Mfanyakazi Stani Katabalo,ambaye naye alikuwa ni Miongoni mwa Waandishi
wanaofanya na Kuandika Habari za Uchunguzi nchini katika kipindi hiko cha
nyuma.
Licha
ya Kubenea kuwa
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Halihalisi pia alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti
hilo la Mwanahalisi.
Katika Kazi za Hatari za kufanya Habari za Uchunguzi Saed Kubenea aliwai
kukumbana na Matatizo ikiwemo kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana na
kupelekea kwenda kutibiwa nje ya nchi ili kuweza kuoka Macho yake ambayo
yalidhulika kwa Tindi kali hiyo aliyokuwa amemwagiwa Usoni hususani kwenye
Macho.
Lakini
mpaka sasa Jeshi la Polisi halijawai kuwataja wala kuwakamata watu waliohusika
na kumfanyia Vitendo hivyo vya kinyama mwandishi huyo nguli katika fani ya
Habari nchini.
Gazeti hilo ambalo lilikuwa lilikuwa
likifichua mambo ya mabaya yaliyokuwa yakifanywa na Serikali,wanasiasa pamoja
Viongozi wa Mashirika mbalimbali hapa nchini,
Hii
ni sehemu ya kwanza ya Sakata la kufungiwa Gazeti hili la mwanahalisi,usikose
tena kesho kujua mengine kuhusu gazeti hilo,ambapo Mtandao huu utakuletea
Simulizi ndefu kwanzia leo tarehe 21 hadi tarehe 25 mwezi siku ambayo ndio
tarehe ya mwisho kuchapisha Gazeti,Nia yetu ni tunataka umma ujue na kufahamu ukweli ulioko
kwenye Sakata la Gazeti hili na Sababu iliyopeleka kufungiwa Gazeti hili,
Tunafanya
hivi labda serikali yetu inaweza kubadilisha mawazo na kuweza kulifungulia
Gazeti hilo ambalo lilikuwa limetoa ajira kwa watanzania wengi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment