Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la
Magereza linafanya uchunguzi kuhusu tukio la kushambalia bus la Magereza namba
T0046 iana ya ISUZU tukio lililotokea tarehe 02.07.2014 maeneo ya Mikocheni karibu na Regency Hotel Kata ya Msasani Wilaya ya Kipolisi ya
Oysterbay Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.
Siku hiyo majira
ya saa 13:30 mchana watu wasiofahamika walilishambulia bus la Magereza
ikiendeshwa na askari Magereza namba A.9716 SGT MUSOFE wakati Bus hilo likiwa
na mahabusu wapatao 15 likitokea Mahakama ya Mwanzo Kawe kupelekwa mahabusu ya
ya Gereza la Segerea wakisindikizwa na askari Magereza pamoja na askari Polisi
kwa wakati mmoja. Ghafla wakiwa kwenye foleni ya magari walitokea watu wawili
wakitembea kwa miguu wakielekea mahali gari lilipo mmoja kati ya watu hao
alianza kufyatua risasi hovyo kuelekeza kwenye gari hilo.
Tukio hilo
lilisababisha kioo cha mbele, cha nyuma, na ubavuni kushoto kuvunjika. Pia askari
03 walijeruhiwa ambao ni A.9716 SGT MUSOFE, Miaka 39, Dereva wa Bus, askari Magereza,
Mkazi wa Segerea ambaye alipata majeraha
kiasi katika mkono wa kulia, Askari wa Polisi wa kike WP.4481 CPL DOTTO askari
Polisi Miaka 33, Mkazi wa Tegete Kanisani
yeye alijeruhiwa kwa risasi kwenye titi lake la upande wa kushoto na
amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na hali yake inaendelea
vizuri. Mwingine ni mahabusu aitwaye DOREEN D/O DAMIAN Miaka 19, Mkazi wa
Tegeta kwa Ndevu ambaye alitibiwa na kuruhusiwa.
Nawaomba
wananchi walisaidie Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi ili watu au kundi
la aina hii ya ujambazi liweze kubainika, wakamatwe na hatimaye wafikishwe
mbele ya mkono wa sheria kama walivyotoa taarifa zilizosababisha kukamatwa kwa
watuhumiwa wa mauaji ya mtawa na tukio la Uporaji katika Benki ya Barcrays tawi
la Kinondoni.
No comments:
Post a Comment