PICHA NA MAKTABA |
Na Karoli Vinsent
KASHFA ya
ufisadi uliofanywa na Serikali ya Rais Jakaya kikwete kwenye Akaunti ya Tegeta
ya Escrow ambayo inadaiwa kuchotwa Bilion
249 na watendaji wa Serikali yake ,sasa yafikia pabaya baada ya leo chama cha
NCCR Mageuzi kuibuka na kusema hakitoweza kukubali ufisadi huo.
Kauli hiyo
imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu mkuu wa Chama NCCR Mageuzi Mosena J Nyambabe ,wakati wa Mkutano
na Waandishi wa Habari,ambapo alisema
chama hicho kimechoka na Ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM,na wameamua
kuanzisha ziara nchi nzima kupinga ufisadi huo.
“Chama chetu
kimeamua kuungana na Mbunge wetu David
Kafulila kuhusu ufisadi huu,kwasababu ushahidi
uko wazi watendaji hawa,wameiba pesa na hizi ni fedha nyingi sana,leo
nchi hii ni masikini haina maji huko vijini,watu wanalala na njaa huko
hospitali dawa hakuna lakini leo watu wachache wanaiba pesa hizi halafu
hawachukuliwi hatua sisi hatutakubali”alisema Nyambabe
Kuhusu spika
wa Bunge kukataa kuunda tume Huru kuchunguza ufisadi.
Nyambabe,alisema
spika wa Bunge Anna Makinda amehusika kwenye ufisadi huu,kutokana na kuendelea
kuwakingia mafisadi hao.
“Namshangaa
Spika huyo kwa kitendo chake kushindwa kuunda tume huru kuchunguza ufisadi huu,kwani kazi ya Bunge ni kusimamia
Serikali,ni aibu kwa Spika kukataa Bunge lisichukue Jukumu lake la kuchunguza
Serikali ,lakini leo anashindwa kufanya hivi,jamani spika huyu hana huruma na
nchi yake?”alihoji katibu huyo
Katibu huyo
alizidi kuendelea kusema kitendo cha Spika Anna Makinda kumwachia mkaguzi mkuu
wa Hesabu za Serikali Ludovick S.l Utouh ni kubariki ufisadi huo wa Ecrow kwani
Mkaguzi huyo aliwai kumsafisha aliyekuwa katibu mkuu wa Wizara ya nishati na Madini Mzee
Jailo.
Kuhusu
Nyaraka asilimia 70 za PAP ambazo ni za kugushi kwenye mkataba wa IPTL.
Katibu huyo
wa chama cha Upinzani kinachokuja kwa kasi nchini alisema ni ujinga kwa
viongozi wetu kwa kushindwa kuona jinsi Mmiliki huyo anavyofoji nyaraka hizo .
“Leo
mwanasheria mkuu wa Serikali anashindwa kuona Jinsi huyu Singa Singa
ambaye ndiye mmiliki wa PAP alinunua
hisa asilimia 70 za IPTL Kwa PIPERLINK kwa 480 milioni”
“kwamba
PIPERLINK ilinunua asilimia hiyo 70 kutoka kwa Merchmar kwa Tsh6 millioni wakati
kampuni hiyo hiyo ilinunua asilimia 30 kutoka kwa VIP alinunua kwa 120bilioni
na pia inaonyeshwa kodi ililipwa disemba 6,2013 wakati fedha alipewa fedha za
esrow tangu Novemba 2013,hivi huyo Spika
haoni Wizi huu”aliongeza Nyambabe
Naye Mbunge
wa Kigoma Kusini David Kafulila ambaye ndio
aliyeibua ufisadi huo wa kutisha alisema Hatomuogopa mtu kuhusu ufisadi
huu licha ya kutishiwa maisha na
Mafisadi hao pamoja na kupelekwa
mahakani ataendelea kulishikia bango sakata hili na kusema watapita nchi nzima
kupinga ufisadi huo na sasa wameanza mkoa wa Kigoma.
Kuhusu kufunguliwa
kesi Mahakani na Mmiliki wa Kampuni ya PAP.
Kafulila,ambaye
ni katibu mwenezi wa NCCR ,alisema atakubali hata kufungwa jela akiwatetea
wananchi wanaoteseka na ufisadi
unaofanywa na Serikali ya CCM.
Ambapo
alizidi kuongeza kwamba Mmiliki wa kampuni ya PAP anayejulikana kama Singasinga, kwani ndiye aliyewai kutajwa
kwenye Mtandao unaoibua Ufisadi wa Wikleaks kwamba ni miongoni mwa watu
waliotajwa kwenye Skendo ya Ufisadi ya Goldenberg nchini Kenya na Jina lake
likiwa no 8 akishirikiana na Mtoto wa Rais mstaafu Kenya,Gidion Moi,na leo
amekuja hapa nchini kufanya ufisadi kushirikina na watendaji wa Serikali huku
akiangaliwa.
No comments:
Post a Comment