Monday, July 7, 2014

HIKI NDICHO WALICHOKIFANYA WAKAZI WA KURASINI LEO


Baadhi ya wakazi wa Mivinjeni ufundi Kurasini wamefunga barabara ya kilwa jijini dar es salaam kwa muda wa saa mbili wakishinikiza kulipwa hundi zao na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka na kusababisha foleni kubwa ya magari.

HABARI24 ilishuhudia sakata hilo ambapo wakazi hao walikusanyika barabarani kwa kile kinachodaiwa kudai hundi zao ambazo walikua walipwe hapo jana baada ya nyumba zao kuthathminiwa.


Wakazi hao wamesema kuwa serikali ilikubaliana na mwekezaji kuwalipa pesa zao na kutaftiwa viwanja huko kibada lakini cha kusikitisha zoezi la ulipaji hundi lilisitishwa hapo jana mpaka waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Prof Anna Tibaijuka atakapotoa tamko lini walipwe.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akiongea kwa njia ya simu na VYOMBO VYA HABARI amemuagiza Mkuu wa Wilaya watu hao kutawanywa na yeyote atakayekaidi atachukuliwa hatua za kisheria kwani si taratibu sahihi kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji barabara hiyo ambao hawahusiki.

No comments: