MAWAKALA watatu wanaojishughulisha na mauzo ya visimbuzi vya
AzamTV wamesafiri kuelekea Brazil kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia.
Mawakala hao ni pamoja na Hasham Lardhi wa kampuni ya SS Hassan,
Al-Farham Dewji wa kampuni ya Regal Solar ya Dar es Salaam na plus Jacob
Mwalyolo wa Maranatha Electronics ya Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Operation Mkuu wa Azam
Media alisema kuwa kampuni hiyo inatambua mchango wa mawakala wake katika
kuendeleza biashara ya visimbuzi hivyo.
Alisema kuwa watakaa Brazil kwa siku kumi kuanzia tarehe 4 mwezi
huu na watapata nafasi ya kuangalia
mechi hiyo ya nusu fainali itakayofanyikia
Belo Horizonte, Julai 8.
Alisema kuwa tangia kuanza kwa biashara ya visimbuzi vya AzamTV mawakala
hao wamefikia kiwango cha juu cha mauzo ya huduma kwa wateja wa Azamtv.
Casse alisema kuwa wakiwa nchini humo watatembelea miji kadhaa
kama vile Rio de Janeiro na Belo Horizonte.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys
Torrington alisema kuwa kwa kipindi hiki cha michuano ya kombe la dunia mauzo
ya visimbuzi vyake yamekuwa makubwa.
Alisema kuwa kwa kutambua mchango wa mawakala katika kufanikisha
mauzo ya visimbuzi vya AzamTV kampuni hiyo itaendelea kuwazawadia mawakala wote
watakaokuwa wakifanya vema.
“Mafanikio yamekuwa makubwa kabisa tangu tumeanza biashara hii
ya kuuza visimbuzi mnamo Desemba mwaka jana na kutokana na mchango wa makawala
tumejitaidi kufanya vema sokoni”.
“Tunawashukuru sana Azam
Media pamoja na mtandao mzima wa biashara ya Bakhresa bila kumsahau Eric Casse ambae tumekuwa tukifanya kazi naye bega
kwa bega kuhakikisha tunafikia malengo yetu kwa ujumla"; kwakweli hii ni
safari ya kipekee katika maisha yetu na tumefurahi sana kupata nafasi ya kwenda
kushuhudia kombe la dunia nchini Brazil, hakika hii ni ndoto iliyokamilika”…kwa
pamoja walisema mawakala hao waliobahatika kupata nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment