Sunday, August 3, 2014

TAIFA STARS OUT AFCON

10s


HATIMAYE safari ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuwania tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Africa, AFCON 2015 nchini Morocco amefia mikononi mwa timu ya taifa ya Msumbiji  ‘Black Mambas’.
Taifa Stars ikiwa ugenini katika dimba la Taifa la Zimpeto nje kidogo ya jiji la Maputo imetandikwa mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano wa kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya AFCON mwakani.
Katika Mechi ya kwanza iliyopigwa wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, vijana wa Mholanzi, Mart Nooij walitoka sare ya mabao 2-2 na leo hii walihitaji kupata ushindi wa aina yoyote ile au sare ya kuanzia mabao 3-3.

No comments: