Friday, August 22, 2014

HABARI ILIYOTIKISA JIJI LEO--KAMISHNA KOVA AUNGURUMA AMWAGA SIMU KWA ALBINO WOTE DAR ES SALAAM,AWAAHIDI NEEMA,ANASA PIA MABILIONI FEKI-CHEKI STORY NZIMA HAPA

Kamishna wa polisi kand maalum ya dar es salaam Suleman kova akimkabidhi mwenyekiti wa chama cha albino Dar es salaam simu kwa ajili ya albino waishio jijini Dar es salaam
  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya D’Salaam limewashauri albino wanaoishi Jijini D’Salaam kuwa karibu sana na Jeshi hilo ili kurahisisha mawasiliano kati yao na Wakuu wa vituo vya Polisi vilivyo karibu na makazi yao au wanapofanyia usalama wao jijini D’Salaam.

       Pamoja na kwamba haijawahi kutoa tukio lolote dhidi ya Albino jijini D’Salaam kutokana na uhusiano uliopo lakini kwa sasa waongeze mawasiliano na Jeshi la Polisi kutokana na taarifa za uhalifu dhidi ya Albino katika baadhi ya mikoa hapa nchini.  
 Pia Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi D’Salaam SULEIMAN KOVA ameongea na Albino hao ofisini kwake na kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi kwa ujumla linaendelea na jitihada kubwa sana kupambana na maadui wa Albino ambao ni wahalifu na wengi wao wameishakamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo wengine wameishahukumiwa.  

         Albino wanatakiwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na Jeshi la Polisi hata kama hakuna tishio la aina yoyote wanalolijua katika maeneo yao ya makazi au wanapofanya shughuli zao za kikazi.

Katika kufanikisha zoezi hilo la mawasiliano ya haraka na Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Kanda Malum ya D’Salaam kwa kushirikiana na wadau kampuni ya SAPNA ELECTRONIC ametoa simu 20 kwa Albino ambao wameudhuria kikao ili iwe rahisi kwao kuwasiliana Jeshi la Polisi kwa namba 0787-668306 ambayo ipo katika chumba cha dharura katika Kikosi cha 999.  

                 Kamishna Kova anaendelea kuongea na wadau mbali mbali ili misaada zaidi ipatikane kwa walemavu wa ngozi ambao ni Albino ili waweze kupata simu za mikononi, mafuta maalum ya kupaka ngozi zao na msaada mwingine wowote ambao utafaa kwa Albino hao kupitia kwa namba 0715 – 009983 hii ni namba ya Kamishna mwenyewe ya oisi na namba nyingine ya Msaidizi wake katika suala la kuwasaidia Albino ni 0756-710179 ambayo ni ya SP. MOSES NECKEMIAH FUNDI.

          Aidha zipo jitihada za makusudi zinazofanyika kati ya Polisi Kanda Maalum ya Polisi D’Salaam na uongozi wa Mkoa na Kitaifa kwa manufaaa ya ulinzi na Usalama wa Albino wote.
        
           Hatua zingine za ziada za muda mfupi na mrefu ni uwepo wa program ya mafunzo maalum kwa Albino wa Jijini D’Salaam ili wapate mafunzo kupitia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa lengo la kupata uelewa wwa kutosha ili nao pia washiriki na kujua namna ya kutoa taarifa kwa lengo la kujikinga na maadui wao ambao wamegubikwa na tama za kujipatia mali, madaraka n.k. kwa njia za ushirikina.

 SABA WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ZA DOLA ZA KIMAREKANI WAKAMATWA
   

              Jeshi  la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za Dolla ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na DOLLA 1,064,000 (Dolla Millioni Moja na Sitini na Nne Elfu) sawa na shilingi za kitanzania 1,702,400,000/= (TSH. Billioni Moja, Millioni Mia Saba na Mbili na Laki Nne) katika nyumba namba 07 walimokuwa wamepanga.

Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam akionyeaha hela feki zilizokamatwa 
                                                                   

Polisi walipata taarifa toka kwa wasamaria wema na kuweka mtego wa kuwakamata ndipo askari walipofika eneo hilo waliwakamata watuhumiwa na noti za USD bandi zikiwa zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo imefungwa kwa namba za siri. 
   
          Aidha watuhumiwa hao walikiri kujihusisha na utengenezaji wa noti bandia, watuhumiwa hao ni kama ifuatavyo;
1.AHMAD S/O MOHAMED Miaka 50, mfanyabiashara, mkazi wa Mombasa Kenya
2.ICHARD S/O MAGOTI Miaka 61, mfanyabiashara, mkazi wa Musoma mkoani Mara.
3.SIMONI S/O LUKIKO Miaka 58, mkazi wa Magomeni Kagera
4.HUMPREY S/O LEONARD Miaka 34, mlinzi, mkazi wa Mburahati
5.FRANK S/O CHARLES Miaka 31 mfanyabiashara, mkazi wa Sinza
6.ABDALLAH S/O YUSUPH,  Miaka 34, mfanyabiashara, Mkazi wa Sinza
7.BAKARI S/O BAKARI,  Miaka 31, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi, Kimara.

     Aidha watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
  

No comments: