Mtendaji mkuu na Msajili Mkuu,wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Philip G,Saliboko Akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita katia ofisi za RITA jijini Dar es salaam |
WAKALA wa
Usajili na ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) inatarajia kufanya tasmini ya mfumo wa Usajili,matukio muhimu ya
Maisha na ukusanyaji wa Takwimu nchini tanzania.
Mfumo huo
ambao utatumika kuchukua taarifa muhimu za vizazi,vifo na Sababu zake,ndoa na talaka.
Akizungumzia
Tasmini hiyo, leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi Habari
Jijini ,Afisa Mtendaji mkuu na Msajili Mkuu,wakala wa Usajili
Ufilisi na Udhamini (RITA) Philip G,Saliboko Alisema Tasmini hiyo itafanyika
kikanda kwa siku kumi na tano (15) kuanzia tarehe 15 Semptemba hadi tarehe 30
mwaka huu na itajumuisha wadau wakubwa wa Masula ya usajili kutoka wizara
,Taasisi,Idara pamoja na Vyuo na wakala Mbalimbali za Serikali.
Waandishi wa habari mbalimbali wakiwa katika mkutano huu ambao umemalizika muda huu jijini Dar es salaam |
Ambapo ameongeza kusema Tathmini itafanywa katika ofisi za Maafisa tawala wa Wilaya,Vituo vya Tiba ,Vituo vya Polisi,nyumba vya kutunzia Maiti,makanisa na kwenye Makazi ya Wananchi ambamo matuko hayo utokea.
Saliboko amewataka Watanzania kutoa ushirikiana mkubwa wakati wa Zoezi hili,kwani ndio njia pekee itakayoisaidia Serikali kufanya mipango yake kikaminifu.
No comments:
Post a Comment