SIKILIZA KIPANDE HICHO HAPO JUU HADI MWISHO USIKIE WAKATI WATANGAZAJI HAO WAKITANGAZA KUZIPOTEZEA HABARI ZA UKAWA KUANZIA LEO
Na Karol vicent
SAA chache kupita Baada Radio ya Clauds Fm kutangaza Rasmi kutozisoma Habari zozote zinazowahusu Wajumbe wanaunda umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA, kwa kile wananachodai Umoja huo hauna jipya bali unataka umaharufu tu.
Na Karol vicent
SAA chache kupita Baada Radio ya Clauds Fm kutangaza Rasmi kutozisoma Habari zozote zinazowahusu Wajumbe wanaunda umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA, kwa kile wananachodai Umoja huo hauna jipya bali unataka umaharufu tu.
Kauli hiyo ya ambayo inakwenda kinyume na Maadili ya Vyombo vya Habari imetolewa leo na Mtangazaji wa Kipindi cha Power breakfast Babra hassani wakati wakichambua magazeti ya siku ambapo alisema kwa sasa hawatazisoma habari zozote zinazohusu umoja huo wa Ukawa kwa madai umoja huo ni wabinafsi na hawana jipya bali wanataka Umaharufu.
Naye Mwanasheria wa Umoja wa kutetea katiba ya Wananchi UKAWA ,Tundu Lissu amewavaa na kusema Radio hiyo inajimaliza na ndio itakuwa inaonekana wazi inapendelea Upande moja Kisiasa.
Kauli hiyo Tundu Lissu,ameitoa mda huu wakati alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu,Kuhusu wao Ukawa wamepokeaje Taarifa hiyo ya kutosomwa Habari zao kwenye Radio hiyo.Ambapo Lissu alisema hizo taarifa anazisikia na kama ni kweli wametangaza hivyo watakuwa wamejimaliza.
“Kwanza nimezisikia hizo taarifa na kama kweli aliyosema huyo mtangazaji ndio msimamo wa Radio nzima basi watakuwa watu wa Ajabu sana maana leo Nchi nzima habari ya Mjini ni Ukawa,leo utasemaje ukawa ni wabinafsi wakati wasomi na watu wengine wanaungana na sisi leo inakuwaje Radio hiyo iseme hivyo kama wako upande mmoja wa Kisiasa weseme”alisema Lissu.
Tundu Lissu,ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba alizidi kusema yeye sio mwanahabari bali anachokijua huo utakuwa msimamo wa Radio nzima na wao Ukawa hawata ogopa na kuacha kuwatetea wananchi kwani wako kwa ajili ya kuwakomboa wananchi na hawezi kukatishwa na tamaa na watu wachache wenye maslai ya upande mmoja.
“Harafu inashangaza sana leo nchi nzima inazungumzia Ukawa harafu mtua aseme leo Ukawa utotangaza habari zao kwa misingi hipi?”alihoji Tundu lissu.
Kauli hiyo ya Tundu Lissu,imetolewa saa chache kupita baada Mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast Babla Hassani,kutangaza Rasmi kwamba hawatasoma Habari zozote zinazohusu Umoja huo.
“Mimi Naona kusoma Story zinahusu Ukawa tunawapa kiki tu wao siwamekuwa kutupotezea kutorejea Bunge I whon doing,vile vikao vinawanufaisha watanzania wote wao ni wabinafsi tu,the best ican do tuwapotezea Habari zao, na ukiona habari inahusu Ukawa tu usisome hapa kwenye Redio,na wakae huko nje atuwataki Ukawa bungeni”alisema Babla Hassani.
Kauli hiyo ya iliungwa Mkono pia na Mtangazaji wa mwengine wa kipindi hicho, Paul Jems anayejulikana kwa jina la Umaharufu “PJ” naye alisema kwanzia sasa hatazisoma habari zozote zinazohusu Umoja huo kwani wanapoteza pesa za wananchi bure kwa kususia bunge hilo.
Msimamo huo wa Watangazaji hao unakwenda Kinyume na Mmiliki wa Radio hiyo ya Clauds Fm Joseph Kusaga alipokuwa anahojiwa na kipindi kimoja cha runinga kutoka nchini Uingereza kinachojulikana,The Sporah Show ambapo katika kipindi hiko alisema Radio yake haina upande wowote wa Kisiasa na kuongeza ni Redio huru inayofanya kazi bila kushabikia upande wowote.
Lakini kwa sasa kauli ya Mmiliki hiyo inakwenda tofauti na ilivyo,na kama Radio ikifanya kama inavyofanya hivyo kwa sasa,Basi Redio hiyo itapelekea machafuko makubwa kama yaliyowai kutokea nchini Rwanda na kuua maelfu ya watu,na sababu kubwa ni Radio za nchini humu zilikuwa na misimamo kama walioyonayo Clauds.
Umoja huo wanaupinga wa Ukawa unaundwa na Muunganiko wa Vyama vikuu vya Upinzani ikiwemo Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Chama cha wananchi CUF,Chama cha Mageuzi NCCR,ND pamoja na Baadhi ya wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Kikwete.
Umoja huo umegoma kurejea kwenye Vikao vya Bunge la katiba kwa madai rasimu inayotokana na Maoni ya wananchi kuchakachuliwa,na kitendo hicho cha Ukawa kimeungwa mkono na wananchi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini pamoja wajumbe wa iliyokuwa tume ya Jaji walioba.
No comments:
Post a Comment