Saturday, August 2, 2014

TUNDU LISSU NA KAFULILA WAIBUKA MDAHALO WA UBUNGO-WATANGAZA RASMI UKAWA KUTOKUINGIA BUNGENI WIKI IJAYO.SOMA HAPA

Tundu lissu akizungumza katika mdahalo huo
 Viongozi wa vyama vya upinzani wanaounda umoja wa katiba Tanzania UKAWA wametoa tamko la kutokuingia bungeni tena katika bunge la katiba linalotakiwa kuanza mapema wiki kesho mjini dodoma.

Akitoa tamko hilo jioni ii katika mdahalo ulioandaliwa na chama cha wanasheria tanzania mbunge kutoka CHADEMA mh TUNDU LISSU amesema kuwa majadiliano yaliyokuwa yanaendelea kati yao na viongozi wa msajili wa vyama vya siasa yamevunjika bila makubaliano yoyote hivyo UKAWA hawatarejea bungeni tena hadi hapo watakaposikilizwa.

"Naomba kutumia mdahalo huu kutangaza Habari ambayo imejiri muda huu na kama wengi mtakuwa hamjasikia ni kwamba majadiliano ya sisi kurejea Bungeni yamevunjika na sisi haturejei tena bungeni bila kusikilizwa hoja zetu"alisema LISSU huku akishangiliwa na mamia ya watanzania waliojitokeza katika mdahalo huo.

Nae mjumbe mwingine wa ukawa DAVID KAFULILA ambaye alipata nafasi ya kuchangia katika mdahalo huo amesema kuwa ukawa kamwe haitarejea tena bungeni bila maridhiano ya kweli ambayo yana maslahi kwa wote.
David Kafulila akichangia katika mdahalo huo

No comments: