Mimi ni bosi wao? Angel di Maria amekuwa mchezaji aliyenunuliwa kwa bei mbaya zaidi kihistoria Uingereza baada ya Manchester United kulipa Pauni Milioni 59.7 Real Madrid
KLABU za Ligi Kuu ya England zimetumia Pauni Milioni 858 baada ya dirisha la usajili msimu huu kufungwa, ambayo ni zaidi ya kiasi kilichotumika kwa klabu za La Liga ya Hispania (Pauni Milioni 425), Serie A ya Italia (Pauni Milioni 260) na Ligue 1 ya Ufaransa (Pauni Milioni 100) jumla.
Hii imeipiku hata Ujerumani ambako klabu zilipoamua kuingia sokoni kwa fujo Bundesliga zilitumia Pauni Milioni 250 jumla pamoja na Pauni Milioni 100 kwa awamu moja ya usajili.
Sehemu kubwa ya fedha inatokana na mikataba ya Televisheni England ambayo inazipa jeuri klabu kusajili kwa bei kubwa na kulipa mishahara minono wachezaji.
Chati hii inaonyesha namna klabu zilivytumia fedha kusajili Ulaya, Ligi Kuu England ikiongoza kwa kutumia Pauni Milioni 857.68
Katika kiasi hicho cha jumla cha fedha, klabu za Ligi Kuu ya England zimetumia Pauni Milioni 520.8 kusajili wachezaji wa kigeni, yaani kutoka née ya Uingereza (England, Scotland and Wales).
Dau kubwa: Usajili wa Eliquiam Mangala (City) na Alexis Sanchez (Arsenal) ump kwenye rekodi ya usajili wa bei mbaya
Pacha wa Blues: Chelsea imefanya biashara ya maana kuwasajili Cesc Fabregas (kushoto) na Diego Costa (kulia)
KLABU IPI IMEFANYA USAJILI BORA?
Manchester United imetumia (jumla ya Pauni Milioni 153.1), na Stoke imetumia (Pauni Milioni 3.4) wakati Southampton imetengeneza faida ya Pauni Milioni 30.7 katika usajili wake.
Chelsea imefanya biashara nzuri yenye thamani halisi ya vipengele vya fedha, ikitengeneza faida na kuboresha timu. Na Leicester na Southampton pia zimefanya vizuri katika thamani halisi kwa kutengeneza timu nzuri kwa gharama kidogo.
Wachezaji walionunuliwa ni pamoja na makipa saba, mabeki 36, viungo 37 na washambuliaji 23
No comments:
Post a Comment