Tuesday, September 2, 2014

FAHAMU ALICHOKIFANYA KAMISHNA KOVA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam SULEMAN KOVA leo akionyesha aina ya silaha ambazo zimekamatwa ndani ya jiji la Dar es salaam kwa wiki hii ambapo amesema kuwa ni harakati za kulifanya jiji la dar es salaam liwe salama na amani itawale ndani ya jiji hili.

Kamishna kova ameendelea kutoa onyo kwa watu ambao wanafanya uhalifu kwa kutumia silaha kuwa sasa mwisho wao umefika kwani jeshi lake sasa halilali kuhakikisha kuwa wanatiwa ndani ya mikono ya polisi.kamishna kova ameyasema hayo leo mchana wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake .

Bastola zaidi ya tano ambazo zilikuwa mikononi mwa wahalifu ambapo polisi kanda maalum wamefanikiwa kuzitia mikononi,jitihada zinaendelea kuhakikisha jiji linakuwa salama
KATIKA HATUA NYINGINE----
JESHI la polisi kanda maalum  jijini Dar es salaam linamshikilia SIMON
MEENA (40)mkazi wa Kinyerezi  Segerea kwatuhuma za kuwasumbua wafanyabiashara mbalimbali  mjini hapa kwa kuwa kuwasingizia pamoja nakuwatuhumu kwamba wanahusika na makosa  yenye kuhatarisha usalama .


Akizungumza na waandishi wa habari jijini mapema hii leo Kamishina wa polisi kanda maalum jijini Dar es salaam Suleiman Kova amesema kuwa kwakipindi kirefu jeshi lake limekuwa likimtafuta mtu huyo baada ya kupata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi nauchunguzi unaonesha kuwa jina lamtu huyo halipo kwenye orodha yawatumishi wa idara ya usalama
wataifa .

‘’Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia
mfanyabishara mwenye asili yakisomali ABDI Mohamed  Dalmar katika tishio hilo la kutishia mtuhumiwa GUNNER SIMON Meena Ambaye ni afisa
  usalama ‘’feki’’ Alidaiwa kiasi chafedha  za kitanzania TSHS 25000,000 amasivyo ange chukuliwa hatua chini ya sheria ya usalama wa taifa
‘’Alisema Suileman Kova .

Kamanda  kova  alisema  baada  ya  mlalamikaji kutoa taarifa katika jeshi lapolisi ndipo jeshi hilo likaweka mtego ilkuweza kufanya uchunguzi zaidi wa shauri hilo  ilkuweza kufikisha mtuhumiwa huyo mahakamani na badaye jalada lake kufikishwa kwa mwanasheria wa serikali . Katika hatua nyingine Jeshi lapolisi kanda maalum jijini Dar es salaam linawashikilia watu tisa kwatuhuma za ujambazi wakiwa na bastola moja aina ya BROWNING ambapo namba zake zikiwa zimefutwa ikiwa na risasi 11
ndani ya magazine huko segerea majira ya saa nane usiku septemba 2
mwaka huu

No comments: