Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF)Absalom Kibanda wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari |
Siku
moja baada ya sakata la waandishi wa
habari kupokea kipigo wakati wakiwa eneo kazi makao makuu ya polisi jana,jukwaa la
wahariri Tanzania(TEF) limeibuka na tamko nzito la kulaani kitendo hicho kwa
kile walihodai kuwa ni mwendelezo wa kuendelea kuwaadabisha wanahabari wakati
wakitekeleza majukumu yao.
Hayo yamesemwa
mda huu Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF)Absalom
Kibanda wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kibanda alisemwa wao
Jukwaa la Wahariri wamesikitishwa kitendo cha Kinyama walichofanyiwa Waandishi
wa habari wakati wa wakati wakitekeleza majukumu yao ya kawaida.
“sisi kama jukwaa la wahariri tumesikitika sana kwa
kile kitendo cha jana na huu ni mwendelezo wa matukio ya kutembeza vipigo kwa
wanahabari wakati wakiwa katika maeneo yao ya kazi”amesema kibanda.
Aidha
jukwaa hilo limewataka jeshi la polisi kufanya mambo kadhaa kabla ya jukwaa
hilo halijachukua hatua zaidi ambapo kati ya mambo hayo ni pamoja na kuwakamata
mara moja askari watatu ambao wanaonekana katika picha wakimshambulia mwandishi
wa gazeti la Tanzania daima Josephat isango.
Pia wamelitaka
jeshi la polisi kufanya ukaguzi wa elimu na uwezo wa askari wao kwa kile
alichosema kuwa kama askari anatambua majukumu yake ya kazi hawezi kufanya
kitendo cha kinyama kama kile cha jana kwa wanahabari hivyo wanamtaka mkuu wa
jeshi la polisi kuhakikisha wanafanya usafi kwa askaria ambao hawana sifa ndani
ya jeshi hilo.
Katika
tukio la jana jeshi la polisi kwa kupitia askari wake walijikuta
wakiwashambulia wanahabari bila kujulikana sababu mara moja ambapo wanahabari
kadhaa walidhurika.
No comments:
Post a Comment