Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi HELEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam |
Ikiwa mchakato wa katiba mpya
ukiendelea kwa bunge maalum la katiba kufikia hatua ya kuipigia kura rasimu
iliyopendekezwa na kisha kuletwa kwa wananchi,imeelezwa kuwa bado watanzania
wengi hususani wale ambao wapo pembezoni mwa nchi hawana uelewa wowote juu ya
mchakato huo na hatua unaopitia.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria
na haki za binadamu LHRC Bi HELEN KIJO
BISIMBA wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu awamu ya pili ya
kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (KAMPENI GOGOTA),kampeni
iliyofanyika katika mikoa ishirini ya tanzania.
Bi HELEN
amesema kuwa katika mikoa mingi waliopita moja ya changamoto kubwa waliyokutana
nayo ni wananchi wengi kukosa uelewa kabisa wa katiba mpya jambo ambali amesema
kuwa linazua hofu kubwa kama
wakipelekewa rasimu iliyopendekezwa kama watakuwa tayari kuipitisha hata kama hawajaelewa na si ile iliyotokana na tume ya
mabadiliko ya katiba tanzania.
Aidha LHRC wamesema kuwa wakati wakiwa kwa wananchi
wamebaini kuwa wananchi wengi wanakosa fursa ya kufwatilia mchakato wa katiba mpya
kutokana na kutokuwa na nyenzo kama television,umeme,radio na nyinginezo huku
akitolea mfano kuwa wilaya ya ngara inasikika vizuri radio moja tu iitwayo
redio kwizera.
Aidha katika hatua nyingene bi HELEN amesema kuwa
wananchi wengi wamekuwa na hofu kubwa ya kutopatikana kwa katiba mpya huku
akisema sababu ni pamoja na kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi
itakayosimamia zoezi la upigaji kura ya maoni na sababu nyingine ikiwa ni bunge
la katiba kuacha kujadili rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi na badala
yake kujadili mambo yao,pamoja na kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa kati ya wajumbe
wa bunge hilo.
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kilifanya
kampeni ya kutoa uelewa kwa wananchi juu ya rasimu ya pili ambapo mikoa ishirini
ilipitiwa ikiwa ni kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment