Ni siku kumi na tano zimepita tangu kuripotiwa tukio la vurugu katika
mdahalo wa Katiba uliohudhuriwa pia na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba Katiba Novemba 2 2014, leo
katika Kikao cha Bunge Dodoma ishu ya walinzi kama wazee kama Warioba
imechukua headlines kwenye maswali na majibu.
Akiuliza swali hilo Mbunge Moses Machari amesema; “…Majuzi
hapa Mzee Warioba tunaelewa wote hapa Wabunge kwamba amefanywa nini
pale Ubungo Blue Pearl Hotel.. Na hapo kwenye swali la msingi la
Mheshimiwa Selasini limezungumzia suala la ulinzi kama umeliangalia
swali hili, sasa waziri unaposimama na kulieleza Bunge kwamba wazee hawa
wanajaliwa vizuri, mambo ya usalama yako sawasawa ni kutowatendea haki
wazee hawa…”
“…Mawaziri
ambao wanatoa majibu ya namna hii tunawafanya nini kwa sababu
wanazungumza uongo ambao uko wazi, hili jambo ni suala la juzi..
Vinginevyo Mheshimiwa Kombani aombe radhi katika suala hili…”– Machari
“…Kwa
hiyo wazee wastaafu wote wanapata ulinzi.. Unless kama ameacha walinzi
wake… Nna uhakika na ninachosema analelewa, anatunzwa na ukitaka
ushahidi nenda kamulize kama hapati facilities zote zinazostahili kwa
viongozi wastaafu…

No comments:
Post a Comment