Mhe Zitto Kabwe
ZITTO KABWE PAMOJA NA KUONESHA UNA UCHUNGU NA TAIFA NIMESHITUSHWA NA WEWE KUUNGA PENDEKEZO LA ANDREW CHENGE AMBAYE NI MTUHUMIWA.
Mara zote watu hudhani nina chuki binafsi na Zitto Kabwe
,Lahasha,Ninampenda sana Zitto Kabwe kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa
kijenga hoja Pamoja na kuwa na ushawishi mkubwa kwa umma.Lakini Pamoja
na hilo,Zitto Kabwe ameliingiza taifa katika kunusuru mafisadi.
Kitendo cha Zitto Kabwe kuunga mkono hoja ya Andrew Chenge kwamba eti mamlaka zilizowateua Mafisadi
kama Prof Muhongo,Pinda,Prof Tibaijuka na wenzake ndizo ziwawajibishe
hivyo kukiuka kabisa mapendekezo ya PAC namba 8,9 10,11,12 ni kubariki
mafisadi kujipa adhabu wenyewe.
Zitto katika pendekezo la Chenge ameunga mkono na kukubaliana huku
akijua Chenge naye ni mtuhumiwa wa scandal hii ya uchotaji wa fedha
katika account ya ESCROW kiasi cha Bilioni 1.6 sawa na milioni 1600 ni
kulinda mafisadi.
Hivi mwizi anaweza kushauri ama kupendekeza adhabu ya kupewa??.Je ni kweli mtuhumiwa anaweza kushauri adhabu kali dhidi yake??
Ona sasa Wabunge wanasema Emmanuel Nchimbi,Hamis Kagasheki,Lowasa nk
waombwe radhi kwa kuwa waliwajibishwa kwa kashfa mbalimbali iweje hawa
walindwe??.Lowasa na wenzake waombwe radhi??
Zitto Kabwe Pamoja na kueleza kwa kina na kwa ufasaha mkubwa,Lakini
kitendo cha kuunga mkono pendekezo la Chenge ni kutuachia maswali mengi
sana yaliyokosa majibu.
Any way,ngoja tukubaliane na wengine pengine ni kutimiza PRINCIPLE OF
NATURAL JUSTICE(NEMO JUDEX IN CAUSA SUA) yaani RIGHT OF RULE OF NO
BIAS..
No comments:
Post a Comment