Tigo
imetangaza leo kwamba imetoa malipo yake ya kwanza ya kila robo mwaka ya kiasi
cha shilingi bilioni 3 (dola milioni 1.8) kwa wateja wake wa Tigo Pesa. Mgao
huu ni wa kwanza kati ya awamu nne za malipo zinazotarajiwa kufanyika kila
mwaka.
Malipo
haya yanafanyka miezi mitatu baada ya kampuni hiyo kulipa kiasi cha shilingi
bilioni 14.25 (dola milioni 8.64) ambacho kilikuwa kimelimbikizwa katika mfuko wa
fedha ya akaunti ya Tigo Pesa, malipo yaliyoifanya Tigo kuwa kampuni ya simu ya
kwanza duniani kuwagawia faida watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa simu za
mkononi. Tigo Pesa ina jumla ya watumiaji milioni 3.6.
Meneja
Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez alisema, “Hii duru ya pili ya kutoa gawio ni
udhihirisho tosha wa muendelezo wa kampuni yetu katika kuwanufaisha wateja na
kuboresha maisha ya Watanzania. Malipo haya yanaenda kwa kila mtumiaji wa Tigo
pesa wakiwemo mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na watumiaji wa kawaida wa
huduma hii. ”
“Gawio
la kwanza lilikuwa kubwa zaidi kwa sababu faida ilimbikizwa kwa muda wa zaidi
ya miaka mitatu na nusu ikilinganishwa na malipo haya ya pili ambayo yanatokana
na malimbikizo ya faida ya fedha zilizohifadhiwa katika mifuko ya benki za
kibiashara kwa muda wa miezi mitatu t kutoka Julai hadi Septemba 2014,” alisema
Meneja Mkuu huyo.
Gutierrez
alieleza kwamba, kama ilivyokuwa hapo awali, malipo wanayopata wateja awamu hii
yanatokana na salio lao la kila siku kwenye akaunti zao za Tigo Pesa. Hii ni
kwa wote; mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na watumiaji wa kawaida.
Mgao
unaofuata wa mwezi Oktoba mpaka Desemba 2014 utalipwa mwezi Februari 2015.
No comments:
Post a Comment