Makamu mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania JUKATA ndugu HEBRON MWAKAGENDA akizungumza na wanahabari mapema leo kuhusu mambo mablimbali yaliyojiri mwaka 2014 |
Jukwa la katiba nchini Tanzania JUKATA limemtaka rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya
Mrisho Kikwete kuwachkulia hatua mara moja wahusika wote waliotajwa kuchota
pesa za account ya TEGETA ESCROW ikiwa ni pamoja na waziri wa nshati na madini
nchini Tanzania Sospeter Muhongo.
Hayo yamesemwa leo jijni Dar es salaam na makamu
mwenyekiti wa jukwaa hilo ndugu HEBRON MWAKAGENDA wakati akizungumza na wanahabari
juu ya matukio mbali mbali ya kikatiba yaliyojitokeza nchni Tanzania kwa mwaka
2014 tukiwa tunaelekea kuuanza mwaka mpya wa 2015.
Amesema kuwa vitendo vya wizi wa mabilioni na ufisadi
mkubwa nchini ni doa kubwa kwa sura ya nchi ambapo rais anapaswa kuchukua hatua
mara moja bila kujali chama wala itikadi,wala urafiki na mtu yoyote.
“lazima
rais awe mkali kama anampenda sana waziri muhongo na anapenda kumpa kazi basi
akampe kazi ya kulima kwenye mashamba yake huko ila sio hii ya kuwaongoza
watanzania kwani imeonekana wazi kuwa ameshindwa kulitumikia taifa”.amesema
makagenda
Aidha akzungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa
uliomalizika hivi karibuni nchini Tanzania amesema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa
na vitendo vya ukiukwaji wa sheria ambapo vilishughudiwa katika maeneo mengi,
na maeneo mengine watu wakitoroka na masanduku ya kura jambo ambalo amesema
kuwa sio ishara nzuri kwa nchi ya kidemocrasia kama hii.
Aidha amesema kuwa vitendo hivi vyote ikiwa ni pamoja
na fujo sizizo na msingi katika
chaguzi,pamoja na ufisadi wa escrow vyote hivi ni kuporomoka kwa maadili kwa
watanzania ambapo amesema kuwa rasimu iliyokataliwa na bunge ilikuwa
inapendekeza vifungu vya maadili lakini vifungu hivyo vyote vimenyofolewa
katika katiba pendekezwa.
Katika hatua nyingne akizunguzia mchakato wa
upatikanaji wa katiba mpya amesema kuwa sasa jukwaa la katiba Tanzania linapendekeza
kuwa hatua zote zilizobaki za mchakato huu ziahirishwe hadi baada ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015,ambapo itakuwa ni jukumu la rais mpya ajaye kuanza upya
mchakato huo,ambapo amesema kuwa sababu kubwa za kuahirisha mchakato huo ni
kutokana na ukweli kwamba Tanzania sasa inakabiliwa na michakato muhimu kama uandikishwaji wa
vitambulisho vya taifa,sakata la escrow,pamoja na uandikishwaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR.
No comments:
Post a Comment