Pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia |
NA KAROLI VINSENT
WAKATI ikiwa Viongozi Mbalimbali wa Vyama vya Kisiasa pamoja na
Wananchi wakiwalahumu Watendaji wa Serikali kwa kufanya makosa na kupelekea
kuwepo na Dosari nyingi kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa ulimalizika Mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Nayo Serikali imeibuka na kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa
Halmashauri mbalimbali nchini na wengingine
ikiwasimamisha kazi kutokana na uzembe waliofanya
uliopelekea kuwepo na dosari nyingi kwenye uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa.
Hayo yametangazwa leo Jijini Dar es Salaam
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa
Ghasia wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo
aliwataja Wakurugenzi waliosimaishwa kazi kutokana na Udhembe
huo ni Felix T.Mabula-kutoka
Hamalshauri,,Fourtunatus Fwema Halmashauri ya Mbulu,Bi Isabella D,Chilumba
kutoka Halmashauri ya Ulanga,Bi Pendo Malabeja kutoka Kwimba pamoja
na Wiliam Z Shimwela kutoka Sumbawanga.
Waandishi Wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza Hawa Ghasia |
Waziri Ghasia aliwataja tena wakurugenzi ambao uteuzi wao
umetenguliwa kutokana na kupelekea Dosari hizo ni Bwana
Benjamini A Mojoro ,Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji Mkuranga,Abdalla
Ngodu,mkurugenzi Mtendaji wa Hamalshauri ya Kaliua,Masalu Mayaya,mkurugenzi wa
Kasulu,Bibi Goody Pamba mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti,Julius A
madiga kutoka Sengerema na Simon CR Mayeye mkurugenzi Mtendaji wa
Bunda.
Vilevile,Waziri Ghasia alisema Serikali pia imewapa Onyo kali
ikiwemo na kuwaweka chini ya Uangalizi na kama ikibainika wana udhaifu Mwingine
Serikali haitosita kuwachukulia hatua ambao ni
Mohamed A.Maje kutoka Halmashauri ya Rombo,Hamis Yuna kutoka
Halmashauri ya Busega pamoja na Jovin A Jungu kutoka Halmashauri ya Muheza.
Hatahivyo,Waziri Ghasia
aliwataja pia Wakurugenzi waliopewa onyo tu ni Isaya Mngulumi kutoka Manispaa
ya Ilala,Melchizedeck Humbe kutoka Manispaa ya Hai pamoja na Wallace J Karia
kutoka Mvomero.
Ambapo
waziri Ghasia alisema uamuzi huo wa kuwafukuza watendaji
hao umetokana na ripoti alizopokea kuhusu masuala yaliyojitokeza
katika uchaguzi huo wa serikali za mtaa na na kwenda kinyume na
sharia ya Ibara ya 36 (1) (4) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977 na Rais ameridhia kuchukuliwa hatua hizo, ambapo pia alisema ni
dhahiri kuwa wakurugenzi wa Halmashauri hizo -
Wameonesha Udhaifu
mkubwa katika kutekeleza Jukumu la Usimamizi wa Uchaguzi ambalo ni moja ya
majukumu ya ukurugenzi.
Alizitaja Kasoro walizofanya Wakurugenzi
hao ni Kuchalewa kuandaa Vifaa vya kupigia kura,kukosa umakini
katika kuandaa Vifaa hasa karatasi za kupigia kura na zengine kuwa na
Makosa,Kuchelewa kupeleka -
Vifaa kwenye vituo vya kupigia kura,Uzembe katika kutekeleza
Majukumu yao pamoja na kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maandalizi wa uchaguzi
kuwa yamekamilika.
Katika Hatua
Nyingine Waziri Ghasia aligoma kujiuzulu na kusema hatua alizochukua ni
wazi kwa wale waliohusika na akalitaka Gazeti la Tanzania
Daima kuandika Habari za Ukweli na kuacha kudanganya Umma.
“Kiukweli nimeshangaa sana na Gazeti la Tanzania
Daima la Jana kusema eti CCM imepoteza zaidi ya Asilimia 80 Mkoa wa
Mtwala,jamani kusema ukweli mimi ni Mbunge kutoka huko ,Halmashauri zote za
Mtwala CCM imeongoza kwa kishindo kikubwa inakuwaje Mwandishi tena uliosomea
kuandika habari ya uongo kiasi hicho”
“Na hili sijui mwandishi wa Gazeti hili alikuwa anamaanisha
nini na kama huyo Mwandishi wa Gazeti hili angekuwa mtendaji wangu
ningemwajibisha kwa kupotosha Umma”alisem Waziri Ghasia
No comments:
Post a Comment